Saturday 3 May 2014

Masaa machache kabla ya KTMA 2014, tuzo za tatu kwa ukubwa Afrika, nani mshindi? 'Itafahamika leo'


Dakika zinahesabika kabla tukio zima la utoaji tuzo za muziki za Tanzania, Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2014 lianze kushuhudiwa na mashabiki wengi waliopiga kura huku joto likipanda kwa baadhi ya wasanii, nani atashinda tuzo katika kipengele husika?
Swali hilo litajibiwa masaa machache yajayo ambapo kila kipengele kitasomwa na mshindi atatajwa huku tukisubiri kuona nani ataondoka na vikombe vingi zaidi (trophies).
Tuzo hizi ni muhimu sana kwa kila msanii aliyetajwa kwenye kipengele husika kwa kuwa ni tuzo kubwa zinazoshika nafasi ya tatu Afrika kwa kuzingatia kuwa nafasi ya kwanza inashikwa na KORA, nafasi ya pili ni tuzo za MAMA (MTV Africa Music Awards).
Kama ilivyo kawaida, tuzo hizo zitapambwa na burudani ya kipekee kutoka kwa wasanii mbalimbali.
 Akiongea katika kipindi cha Sun Rise cha 100.5 Times Fm, Meneja wa bia ya Kilimanjaro, George Kavishe aliahidi kuwa kutakuwa na burudani ya kipekee hata zaidi ya ile ya mwaka jana iliyokuwa gumzo pale wasanii wakongwe walipoimba nyimbo za wasanii wa kizazi kipya huku wasanii wa kizazi kipya wakiperform nyimbo za wasanii wakongwe.
Utoaji wa tuzo hizo utaoneshwa Live kupitia vituo vitatu vya runinga chini na kupitia tovuti ya Kilimanjaro Premium Lager.
Mitandao ya kijamii pia itakuwa sehemu kubwa ya media. Fuatilia Times Fm katika Twitter  @timesfmtz na katika instagram @timesfmtz ama Facebook Times Fm Tz.

No comments:

Post a Comment