Thursday, 24 April 2014

ANGALIA BAADHI YA WASANII WANAOSADIKIKA WANAPENDWA ZAIDI TANZANIA



                          

Ukiachilia mbali wingi wa wasanii wanaofanya vizuri kwenye tasnia mbali mbali apa bongo, sio wote wanaobahatika kukubalika na kupokelewa vizuri na Jamii/mashabiki. Hawa wanasadikika ndio wasanii wenye mvuto zaidi  kwa kupendwa na mashabiki.


                                                                    1.DIamond platinum

Anaweza akawa sio muimbaji mzuri kama Alikiba au barnaba, ila haina ubishi huyu ndiye msanii wa kiume kwa upande wa bongo fleva anayeongoza kwa kupendwa zaidi na mashabiki, jina lake linazidi kukua siku hadi siku na kazi zake zinafanya vizur karibia east Africa nzima.

                                                                  2. Wema sepetu
Sio muigizaji mzuri kumshinda Johari, wala hana filamu nyingi sokoni kuliko Irene uwoya, ndio maana hata waandaji wa tunzo za filamu hawajawahi kum nominate hata kwenye category ya msanii chipukizi bora, hiyo haijafanya jina lake lishuke kwenye Tasnia hiyo, Bado haina ubishi wema ana nyota Kali na anapendwa kuliko msanii yeyote. mwenyewe anajiita ENDLESS FAME.

                                                           3. LADY JAYDEE
Kiuno chake kina mfupa, hana mauno makali kumzidi Snura mushi, sauti yake nzuri na kipaji cha pekee alichobarikiwa kimemfanya apendwe zaidi na mashabiki kibao. Unadhani ana pesa sana kuliko ruge? Hakustahili kabisa kushindana naye , ila jeuri ya mashabiki aliyonao ilimfanya ajione malkia , nadhan unakumbuka Team anaconda ilifanya nini pale Nyumbani Lounge. Jide ana nyota Kali sana.

                                                                              4. JB
 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgIhyphenhyphenh3mziRN3C7nZDvsQv6Z147OVD8rRsPCFqNuzW7_RW8XekqCaPbpIv5tLwg0rJ4nvGh2mrqZU7iNh36f8rDnQNIwPhG8HfcWZBQmLkddYsFUMdkiHETYsyI8_0K_DpngwZ_sWA8jmLu/s1600/JB_23.JPG
Kipaji chake hakikumfikia marehemu kanumba(r.I.p),sio director mzuri kama Jackson kibirigi, ubunifu alionao kwenye filamu zake umemfanya apendwe zaidi na mashabiki kuliko msanii yeyote wa kiume kwa upande wa filamu apa bongo.


                                                                     5.Lulu Michael
 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiKW_Ym-IyDr-7okyFovOxVZhHhTJ6nrk6XKO5CzwwlB8r_3fdigPvmtfGwYkomCd0TB5SWaxpzUAHnPnsbr1YgIzpIVZPj1bFpH_UVEMN6XX9sBF81kcxCfeFWzrCxuOKzoazQF-o1iLr5/s1600/1926692_696517747037658_409001088_n.jpg

Hajawahi kuigiza vizuri kama Diana kimaro(Danija,Kigodoro) ila ana nyota nzuri sana, licha ya umri mdogo alionao , anapendwa na ana mashabiki wengi zaidi.

                                                                      6.Monalisa
 http://www.bongo5.com/wp-content/uploads/2012/12/Yvonne-Cherryl-Monalisa-480x511.jpg


Hana umbo kama masogange, kipaji cha kipekee alichonacho na umakini alionao kwenye uigizaji umemfanya ajiongezee mashabiki wengi zaidi.

                                                                           7. Ray kigosi
Sio muigizaji mzuri kumshinda Gabo, kampuni makini aliyonayo na aina ya waigizaji anaowatumia imemfanya kazi zake zinunuliwe zaidi kuliko kampuni yeyote apa bongo. Steps ilishawahi kusema kuhusu kazi za waigizaji zinazonunuliwa kama njugu, ray alishika namba mbili akitanguliwa na kanumba.

                                                                           8.Johari

Hana swagger kama wema sepetu, kazi zake na umakini alionao kwenye uigizaji , vimemfanya apendwe zaidi na mashabiki , ndo maana hadi Leo kazi zake zipo juu.

PICHA ZA KWANZA ZA HARUSI YA P-FUNK MAJANI



                                      Maharusi P Funk & Hidya mara baada ya kufunga ndoa



DRAKE AMNUNULIA RIHANNA PETE YENYE THAMANI 68 MILIONI



            
Drake na Rihanna penzi lao linachanua huku wakiripotiwa kuwa na mpango wa kuishi pamoja.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Star, chanzo kimoja kimeeleza kuwa Drake amemnunulia Rihanna zawadi ya pete ya almasi yenye rangi ya njano yenye thamani ya $42,000 (sawa na 68,712,000/-).


Hata hivyo imeelezwa kuwa pete hiyo sio ya uchumba.
“Rihanna aliikubali zawadi hiyo kama ishara ya mapenzi ya Drake. Sasa hivi (Drake) anabadili hata ratiba zake ili atumie muda mwingi ipasavyo kuwa na Rihanna.” Kilieleza chanzo hicho.


Drake na Rihanna wanaonekana kuwa karibu zaidi kadiri siku zinavyozidi kwenda, na hata Jumapili katika MTV Movie Awards walionekana wakiwa wameshikana mikono muda mfupi baada ya Drake kuperform.

RAPPER AJARIBU KUJIUA KWA KUJIKATA UUME




Rapper wa Marekani, Andre Johnson aliyejaribu kujiua kwa kujikata uume wake aliwashangaza wengi kwa kuwa kitendo hicho sio cha kawaida na wengi walitaka kufahamu sababu hasa iliyompelekea kufanya jaribio hilo. 

Kwa mujibu wa E! News, chanzo cha kuaminika kimeeleza kuwa rapper huyo alitumia madawa hatari ya PCP ambayo yanajulikana kama Phencylidine au Angel Dust kabla ya kufanya tukio hilo na kujaribu kujirusha kutoka kwenye balcony baada ya polisi kufika na kumuomba ashuke aongee nao. 

PCP yanatajwa kuwa moja kati ya madawa ya kulevya hatari zaidi na humfanya mtu kuwa na hasira na kufanya uharibifu na hupelekea watu kujifanyia mambo ya hatari zaidi. 

Japokuwa rapper huyo alilkubali ombi la polisi hao, alijiachia ghafla hadi chini. Polisi walipoingia ndani ya nyumba walikuta kipande cha sehemu ya uume wa rapper huyo. 

Kutokana na hali mbaya aliyokuwa nayo, alikimbizwa hospitalini ambapo alipewa huduma. 

Hata hivyo, madaktari walishindwa kabisa kuunganisha uume wake.

RIHANNA ASHEREHEKE UVUTAJI BANGI


Muimbaji Rihanna aungana na wenzake kusherehekea sherehe ya uvutaji bangi

CHRIS BROWN HATARINI KWENDA JELA CHRIS BROWN HATARINI KWENDA JELA





Kesi ya Chris Brown inaanza kuwatia wasiwasi mashabiki wake kuwa huenda hali ikawa mbaya kwa muimbaji huyo baada ya mlinzi (bodyguard) wake kukutwa na hatia katika kesi iliyomkabili ya kumshambulia mtu akiwa na Chris Brown. 

Jaji Patricia Wynn ambaye anaendesha kesi ya mlinzi huyo na ya Chris Brown amesema mlinzi huyo amekutwa na hatia kutokana na ushahidi uliotolewa na dereva. 

Dereva huyo ameeleza mahakamani hapo kuwa Chris Brown alimpiga Adams na baadae mlinzi wake akaingilia na kumshambulia pia. Jaji ameeleza kuwa kitendo cha mlinzi huyo hakikuwa sahihi kwa kuwa hakuna ushahidi wowote unaoonesha kuwa kijana huyo alikuwa amemsogelea Chris Brown. 

Mwanafunzi mwingine wa Howard University, Jalen Garrison aliongeza kuwa yeye na rafiki yake walikuwa wanapiga picha na Chris Brown wakati ambapo Adams ambaye ni boyfriend wake alijaribu kupiga picha na mkali huyo wa With You. Lakini Chris Brown aliwaka na kumtolea maneno ya lugha chafu kabla hajampiga usoni. 

Adhabu ya mlinzi huyo imepangwa kutolewa June, 25. Mlinzi huyo alikiri kuwa alimpiga mtu huyo na alijitetea kuwa alimpiga kwa nia ya kumlinda Chris Brown. 

Chris Brown pia amepangwa kusimama kizimbani Jumatano, April 23 kwa kesi hiyo

Tuesday, 15 April 2014

SHETA ASIMULIA ALIVYOPATA AJALI



MWISHONI mwa wiki  iliripotiwa juu ya msanii Shetta kupata ajali mbaya ya gari wakati akielekea Babati, mkoani Manyara kwa ajili ya kazi za muziki ingawa aliweza kunusurika katika ajali hiyo.
Akizungumza na Pro-24 msanii huyo alielezea kisa kizima kilichopelekea kutokea kwa ajali hiyo mkoani huko ambapo ilisababisha kazi hiyo ya muziki kushindwa kufanyika mkoani hapo.
Alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ilikuwa ni kumkwepa Pundamilia aliyekuwa akikatiza barabarani hali iliyopelekea kpata ajali mbaya ingawa anamshukuru mungu kuwa hivi sasa yupo salama.
"Nilitumia usafiri wa ndege kutoka Dar es Salaam, hadi Arusha ambapo nilikuwa na kazi huko Babati kufika sehemu inayoitwa Minjingo ambapo sehemu hiyo inakuwa na wanyama wengi kidogo , tulikutana na Pundamilia mmoja barabarani alikuwa ameshavuka sasa wakati gari pia haijavuka nae alikuwa anataka kurudi tena huko halafu gari lilikuwa kwenye mwendo kasi kidogo" alisema Sheta.
Sheta ameeleza kuwa gari limeumia sana lakini wao wamenusurika ingawa bado anamaumivu ya kawaida ambapo hivi sasa yupo hospitali kwa ajili ya kupima afya yake kama anamaumivu yoyote ndani .
Ameweka wazi kuwa kutokana na ajali hiyo imebidi show yake iahirishwe kwa kuwa kila mtu alikuwa amepata taarifa kuhusu ajali hiyo hivyo hakuwa na sababu yoyote ya kuendelea na show hiyo zaidi ya kuimarisha afya yake kwanza.

JOTI AFUNGUKA KUHUSU MAIGIZO


              Lucas mhuvile
Mchekeshaji mahiri katika tasnia ya filamu Bongo Lucas Mhuvile ‘Joti’ amesifia kurudi kwa kundi la Kaole na kufanikiwa kutengeneza tamthilia kali nay a kusisimua ya Kipusa, Joti amedai kuwa wasanii walitoka na kufanikiwa kwa sababu walimudu katika maigizo na si katika filamu.

“Nimefurahi sana hasa kwa Kipemba kunialika na kuona kazi yenye ubora mkubwa sana, niseme ukweli huku ndio kwetu, sisi wenyewe tumetoka katika maigizo na tulifanya vizuri, katika filamu bado ndio maana hazifanyi vizuri nje ya nchi,”alisisitiza Joti.
             ZE COMEDY 538
Joti amewaomba wasanii walitoka katika makundi ya maigizo kurudi huko na kutengeneza tamthilia zitakazoelezea maisha halisi ya Watanzania kama ilivyokuwa hapo awali , kama yaliyokuwa na ushindani kama Nyota Nsemble, Kidedea, Splendid sanaa itarudi na kufanya vizuri
KWA HISANI YA FC

DUDE ASEMA "BONGO MOVIE HAKUNA UPENDO"


             Kulwa Kikumba 532 b
Kulwa Kikumba ‘Dude’ Mtayarishaji na muongozaji wa filamu Bongo amewashukia wasanii wa filamu maarufu kama Bongo Movie kuwa hawana upendo wala utu zaidi ya kuangalia maslahi yao au njia ya kutengeneza fedha tu lakini siyo kutoa misaada ya kweli kwa jamii na wazazi wa wasanii waliofariki.

“Bongo Movie kumetoa taswira mbaya katika tasnia ya filamu, Visasi, chuki, ubinafsi, ugomvi, ndivyo vilivyotawala huku ubora wa filamu ukiwa umeporomoka kama si kushuka kupita kiasi hakuna ubunifu,”
“Sharo, Kanumba na Sajuki tumewasahau hakuna anayewakumbuka, kama leo mama Kanumba kaamua kuigiza usishangae mama Sharo naye akiingia kuigiza ili maisha yaende,”anasema Dude.

Dude anasema kuwa ipo haja ya kuangalia na kuiokoa tasnia ya filamu inayoekea kuzama katika kwa kasi kama vile katika mkondo hatari wa Bahari Nugwi

Thursday, 3 April 2014

Diamond afanya wimbo na Dr Sid wa Nigeria

Safari ya Diamond nchini Nigeria inaendelea kuzaa matunda kama alivyokusudia. Baada ya kushirikishwa na Waje, jana mkali huyo wa bongo flava aliingia booth na msanii mwingine mkubwa wa Nigeria, Dr Sid. Jana usiku Dr SID amepost kwenye Instagram picha akiwa studio na Diamond na kuandika, “Studio Session with @diamondplatnumz #AfricanPrince #NaijaTanzania”

na ushindi wa tuzo za KTMAs 2012 & 2013, mwaka huu pia wanawania

Warriors From the East walivyofaidikaKundi la muziki wa reggae lenye makazi yake jijini Arusha, Warriors From the East ambalo liliwahi kushinda tuzo mbili za Muziki za Tanzania zinazotolewa kwa udhanimi wa Kilimanjaro (KTMAs) wameeleza jinsi ushindi wa tuzo hizo miaka miwili iliyopita ulivyowafaidisha kimuziki.

Kiongozi wa kundi hilo, Magere ameiambia tovoti ya Times Fm kuwa ushindi wa tuzo hizo mwaka 2012 na 2013 uliwatambulisha zaidi kwenye maeneo mbalimbali Tanzania na kupata shows, deals na promotion zaidi hata nje ya nchi.
“Kabla ya hapo tulikuwa tunafahamika tu mkoa wa Arusha, Moshi na zile sehemu mbalimbali tulikuwa tunaenda kama Mwanza, Zanzibar na Dar es Salaam kwa wale tu wapenzi wa reggae, maaana tukiandaa show ladba Dar es Salaam wale fans wa reggae ndo wanakuja kwenye show, lakini baada ya kushinda tuzo ile iliweza kutufikisha kwa kila mwana jamii.” Amesema Magere.
Ameeleza kuwa baada ya kuzibeba tuzo hizo hata promotion yao kwenye media iliongezeka na watu wakazidi kuwaona tofauti na zamani.
“Imeweza kutupa utambulisho kwa jamii ya Tanzania na hadi nje ya nchi. Tukienda kule Uganda, tukienda Kenya ama tukienda Ethiopia tunatambulika kwamba hawa ndio washindi wa tuzo za Kilimanjaro Music Awards kule wa wimbo bora wa reggae.” Ameeleza kiongozi wa Warriors From the East.
Mwaka huu pia kundi hilo limepata nafasi ya kuwania tuzo hizo kwenye kipengele cha wimbo bora wa reggae na wimbo wao ‘Bongo Reggae’.
“Mwaka huu tena mashabiki wameamua kutuchagua tuwanie tuzo…njia ya kutupigia kura, njia kuna njia tatu. Njia ya kwanza ni kwa SMS, andika herufi AD5 kisha unatuma kwenda namba 15440. Njia ya pili unaenda kwenye Website za Kilimanjaro ambazo ni www.kilitime.co.tz utakuta kuna wimbo bora wa reggae unatupigia kura. Na njia ya tatu ni njia ya Email, ambayo ni ktma@audiotaxinternational.co.tz

Drake ajibu diss ya Jay Z 'Mrs Dreezy' kwenye wimbo wake mpya Draft Day,

Hivi karibuni mashabiki wa Drake na Jay Z walipata mshituko baada ya Jay Z kumdis Drake kwa kumuita Mrs. Dreezy kwenye wimbo alioshirikishwa na Jay Electrica ‘We Made It’. Mshituko ulitokana na jinsi ambavyo wawili hao walikuwa karibu. Diss ya Jay Z kwa Drake ilitokana na comments zilizodaiwa kutolewa na Drake kwenye jarida la Rollingstone kuwa hawezi kwenda bars nne bila kuimba kuhusu sanaa za uchoraji, comment ambayo Drake aliikana baadae.
Jana, Drake aliachia wimbo wake mpya ‘Draft Day’ aliosample wimbo wa Lauryn Hill ‘Doo Wop (That Thing)’, ambapo alisikika kwenye wimbo huo kama anajibu diss ya Jay Z kumuita Mrs Dreezy ‘Sorry Mrs Dreezy for so much I talk…’
Drake amejibu mstari huo kuwa amejikita katika kutengeneza nyimbo kali na kukua zaidi, na kwamba hakuna u-Mrs..
“I’ focused on making records and getting’ bigger
Just hits, no misses (Mrs), that’s for the married folk.” Amerap Drake.
Hata hivyo, rapper huyo amejaribu kuonesha kuwa sio vibaya kutumia sanaa ya uchoraji kwenye mistari na hivyo kuifuta kauli iliyoripotiwa na Rollingstone iliyomkera Jay Z.
“I think I’m on my eighth flow, just watch me paint flow
We all do it for the art so I can never hate though.” Amesikika Drake kwenye Draft Day.
Drake amevunja kauli yake aliyowahi kusema kuwa “Diss me and you’ll never hear a reply to it.” Haijafahamika bado kama hii ni hali ya kuchangamsha game na kumpa kick Drake ama ni uhalisia wa sema nikujibu kati ya mkongwe Jay Z na rapper huyo wa YMCMB.

2Chainz kupandishwa kizimbani kwa kesi ya dawa za kulevya

Rapper 2 Chainz atapandishwa kizimbani wiki ijayo kujibu mashitaka kufuatia tukio la kukamatwa na codeine inazotumika kutengeneza dawa za kulevya aina ya sizzurp, June mwaka jana.
 Kwa mujibu wa TMZ rapper huyo wa Georgia baada ya kukamatwa mwezi June polisi waliripoti kuwa mbali na codeine alikutwa na dawa nyingine za kulevya ikiwa ni pamoja na bangi.
Endapo atakutwa na hatia katika kesi hiyo, 2Chainz anaweza kutumikia kifungo cha hadi miaka mitatu jela.

Tuesday, 1 April 2014

Diamond Kwenye Tuzo Kubwa Africa,Kilio Chake Kikubwa Kwako Kiko Hapa!

Msanii Diamond Platnumz, ameendelea kuchana mawimbi katika anga la muziki hususan kwa upande wa Afrika ambapo amefanikiwa kuingia katika orodha ya wasanii 20 Bora ambao wanafanya vizuri Afrika, ambao wataingia katika kinyanganyiro cha kuwania tuzo za Kora.

Diamond katika orodha hii, anatokea sambamba na majina ya wasanii wakubwa Afrika, kama vile Oliver Mtukudzi, Fally Ipupa, Mafikizolo pamoja na wakali wengine wa muziki barani Afrika.
Kutokea kwa Diamond katika orodha hii, ni nafasi nyingine kubwa ya kuipeperusha bendera ya Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla, katika jukwaa la kimataifa.
Kwa sasa mchakato unaendelea kupitia ukurasa wa facebook wa Tuzo hizi, ambapo maoni mbalimbali ya mashabiki yanakushanywa kuhusiana na wasanii gani wanaokubalika zaidi, tayari kwa kuwapambaniza katika tuzo hizo kubwa.
dd 2dd

2Chainz ampa msichana umaarufu kwa usiku mmoja, msichana huyo amshtaki baada ya kuona video ya tukio


Ni vigumu sana kwa mtu wa kawaida kupata nafasi ya kuingia kwenye chumba cha maandalizi au sehemu maalum ya maandalizi nyuma ya jukwaa ya staa kama 2 Chainz na kuuza sura. Nafasi hiyo aliipata msichana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Tina.
Msichana huyo aliingia kwenye chumba hicho na kula pozi akiwa amepewa sapoti ya kufanya hivyo na watu wa karibu wa 2Chainz ambao alidai kukutana nao kwenye Instagram, lakini pia alijikuta akipiga story na 2Chainz mwenyewe huku akirekodiwa katika video.
Baada ya maongezi ya dakika , watu wa 2Chainz walimfahamisha kuwa kila kitu kinarekodiwa na kwamba hapo back stage palikuwa ni sehemu ya watu wa blogs.
Msichana huyo alijiweka poa na kuongea mawili matatu huku akijipa shavu kwa watu wamfuate kwenye Instagram.
“Aww sh*t! This is going on a blog, for real?! This is going on a blog and you’re really recording? Do I look good? You guys can follow me at Iluvtinaa on Instagram.” Alisema Tina huku akiiangalia kamera.
Baada ya utani na kumpongeza 2Chainz kwa show yake aliamriwa kuondoka eneo hilo.
Lakini baada ya 2Chainz kuiweka kwenye mtandao video ya tukio zima mambo yaligeuka na msichana huyo hakupenda kabisa jina ambalo video hiyo ilipewa, maandishi yaliyomtaja yeye kama kahaba kwa neno ‘THOT’ (That H*e Over There).
‘#isthisYoThot’ iliandikwa video hiyo.
Msichana huyo aliandikwa kwenye Instagram kuwa amechukizwa na kitendo alichofanyiwa na 2Chainz na kwamba anatamani 2Chainz angejisikia kama alivyojisikia vibaya na kudai kuwa ameshaanza kufanya utaratibu wa kumfungulia mashitaka.
“Niko kwa mwanasheria wangu muda huu, namalizia taratibu za kisheria, jiandae kwa kesi, hauna haki ya kuvuruga maisha yangu na kunichafua kama hivi. Sasa wote mtajibu kwa hili.” Ilisomeka sehemu ya ujumbe wa Tina kwenye Instagram

MAFANIKIO YA LUPITA



Siku zote katika maisha inapotokea mafanikio kwa mtu au jambo la ushindi, kila mmoja wetu hutumia muda wa kusifia tukio hilo huku na sisi tukitumia muda huo katika kuponda wale ambao tunahisi hawajafanya kitu katika tasnia ya filamu, hilo limekuja baada ya binti mzaliwa wa Mexico na raia wa kenya Lupita kujizolea tuzo za Oscar.



Nimeona ujumbe mbalimbali katika mitandao ya kijamii kuna watu wametoa hisia zao, lakini kuna wakati ambao huwa tunashambuliana wenyewe kwa wenyewe bila kuangalia mwanzo wa tatizo letu la asili, ambalo ni kukosekana tuzo tu za ndani ambazo ndio kichocheo.


Lakini wakati tunaona yale ya Lupita Nyong’o mtoto wa Profesa na mazingira ambayo yalimfikisha hapo tunaangalia watoto wa wakulima kama Jackson Kabigiri ambaye hata shule yake alisoma hapa hapa hakupata mwanga zaidi kufika mbali na kusoma marekani aliposoma Lupita?
        

Asili ya mafanikio na kufika mbali pia uchangiwa na upendo, uelewa na fursa kwa mzazi, ambalo Lupita pamoja na baba yake kuwa mwanasiasa mkubwa bado hakuona sababu ya kumshawishi mwanaye ajiingize katika siasa ili wajenge familia ya kisiasa na kupokezana uongozi katika nyanja za kisiasa.


Ninaposema upendo maana yangu ni kwamba kama baadhi ya vijana ambao wamekuwa wakipigania tasnia hii ya filamu kwa muda mrefu nao wakafunguliwa na kuwa na mwanga na kubaini mambo yanavyokwenda ulimwenguni basi nao ingekuwa ni kitu cha kujivunia


Bongo tuna wasanii wengi sana ambao mfumo kwao umekuwa tatizo, niliamua kumuongelea Jackson Kabirigi kwa sababu ndiye msanii ambaye kwa mwaka 2013 kwa kiwango cha bongo aliweza kufika mbali hadi filamu kuibuka kama filamu bora ya kiasili.

         
Nilitegemea sana kuongelewa na kila chombo kama ni sehemu ya kutambua juhudi kidogo dogo zinazofanywa na wasanii wetu pamoja na kuwa na uwezo mdogo katika ushiriki wa matamasha ya kimataifa, pale kinapoonekana kidogo kitolewa ushabiki kama watu walivyoshabikia kwa Lupita.
          

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alikuwa bega kwa bega kumtia moyo Lupita kwani alikuwa akifuatilia mchakato wa tuzo hizo kwa kutuma ujumbe katika mitandao ya kijamii, lakini hapa kwetu pamoja na filamu ya mdundiko kurudi na ushindi sina hakika hata kama kuna kiongozi wa filamu alitoa pongezi kwa ushindi huo