Jana, Drake aliachia wimbo wake mpya ‘Draft Day’ aliosample wimbo wa Lauryn Hill ‘Doo Wop (That Thing)’, ambapo alisikika kwenye wimbo huo kama anajibu diss ya Jay Z kumuita Mrs Dreezy ‘Sorry Mrs Dreezy for so much I talk…’
Drake amejibu mstari huo kuwa amejikita katika kutengeneza nyimbo kali na kukua zaidi, na kwamba hakuna u-Mrs..
“I’ focused on making records and getting’ bigger
Just hits, no misses (Mrs), that’s for the married folk.” Amerap Drake.
Hata hivyo, rapper huyo amejaribu kuonesha kuwa sio vibaya kutumia sanaa ya uchoraji kwenye mistari na hivyo kuifuta kauli iliyoripotiwa na Rollingstone iliyomkera Jay Z.
“I think I’m on my eighth flow, just watch me paint flow
We all do it for the art so I can never hate though.” Amesikika Drake kwenye Draft Day.
Drake amevunja kauli yake aliyowahi kusema kuwa “Diss me and you’ll never hear a reply to it.” Haijafahamika bado kama hii ni hali ya kuchangamsha game na kumpa kick Drake ama ni uhalisia wa sema nikujibu kati ya mkongwe Jay Z na rapper huyo wa YMCMB.
No comments:
Post a Comment