Tuesday, 1 April 2014

2Chainz ampa msichana umaarufu kwa usiku mmoja, msichana huyo amshtaki baada ya kuona video ya tukio


Ni vigumu sana kwa mtu wa kawaida kupata nafasi ya kuingia kwenye chumba cha maandalizi au sehemu maalum ya maandalizi nyuma ya jukwaa ya staa kama 2 Chainz na kuuza sura. Nafasi hiyo aliipata msichana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Tina.
Msichana huyo aliingia kwenye chumba hicho na kula pozi akiwa amepewa sapoti ya kufanya hivyo na watu wa karibu wa 2Chainz ambao alidai kukutana nao kwenye Instagram, lakini pia alijikuta akipiga story na 2Chainz mwenyewe huku akirekodiwa katika video.
Baada ya maongezi ya dakika , watu wa 2Chainz walimfahamisha kuwa kila kitu kinarekodiwa na kwamba hapo back stage palikuwa ni sehemu ya watu wa blogs.
Msichana huyo alijiweka poa na kuongea mawili matatu huku akijipa shavu kwa watu wamfuate kwenye Instagram.
“Aww sh*t! This is going on a blog, for real?! This is going on a blog and you’re really recording? Do I look good? You guys can follow me at Iluvtinaa on Instagram.” Alisema Tina huku akiiangalia kamera.
Baada ya utani na kumpongeza 2Chainz kwa show yake aliamriwa kuondoka eneo hilo.
Lakini baada ya 2Chainz kuiweka kwenye mtandao video ya tukio zima mambo yaligeuka na msichana huyo hakupenda kabisa jina ambalo video hiyo ilipewa, maandishi yaliyomtaja yeye kama kahaba kwa neno ‘THOT’ (That H*e Over There).
‘#isthisYoThot’ iliandikwa video hiyo.
Msichana huyo aliandikwa kwenye Instagram kuwa amechukizwa na kitendo alichofanyiwa na 2Chainz na kwamba anatamani 2Chainz angejisikia kama alivyojisikia vibaya na kudai kuwa ameshaanza kufanya utaratibu wa kumfungulia mashitaka.
“Niko kwa mwanasheria wangu muda huu, namalizia taratibu za kisheria, jiandae kwa kesi, hauna haki ya kuvuruga maisha yangu na kunichafua kama hivi. Sasa wote mtajibu kwa hili.” Ilisomeka sehemu ya ujumbe wa Tina kwenye Instagram

No comments:

Post a Comment