Warriors From the East walivyofaidikaKundi la muziki wa reggae lenye makazi yake jijini Arusha, Warriors From the East ambalo liliwahi kushinda tuzo mbili za Muziki za Tanzania zinazotolewa kwa udhanimi wa Kilimanjaro (KTMAs) wameeleza jinsi ushindi wa tuzo hizo miaka miwili iliyopita ulivyowafaidisha kimuziki.
Kiongozi wa kundi hilo, Magere ameiambia tovoti ya Times Fm kuwa ushindi wa tuzo hizo mwaka 2012 na 2013 uliwatambulisha zaidi kwenye maeneo mbalimbali Tanzania na kupata shows, deals na promotion zaidi hata nje ya nchi.“Kabla ya hapo tulikuwa tunafahamika tu mkoa wa Arusha, Moshi na zile sehemu mbalimbali tulikuwa tunaenda kama Mwanza, Zanzibar na Dar es Salaam kwa wale tu wapenzi wa reggae, maaana tukiandaa show ladba Dar es Salaam wale fans wa reggae ndo wanakuja kwenye show, lakini baada ya kushinda tuzo ile iliweza kutufikisha kwa kila mwana jamii.” Amesema Magere.
Ameeleza kuwa baada ya kuzibeba tuzo hizo hata promotion yao kwenye media iliongezeka na watu wakazidi kuwaona tofauti na zamani.
“Imeweza kutupa utambulisho kwa jamii ya Tanzania na hadi nje ya nchi. Tukienda kule Uganda, tukienda Kenya ama tukienda Ethiopia tunatambulika kwamba hawa ndio washindi wa tuzo za Kilimanjaro Music Awards kule wa wimbo bora wa reggae.” Ameeleza kiongozi wa Warriors From the East.
Mwaka huu pia kundi hilo limepata nafasi ya kuwania tuzo hizo kwenye kipengele cha wimbo bora wa reggae na wimbo wao ‘Bongo Reggae’.
“Mwaka huu tena mashabiki wameamua kutuchagua tuwanie tuzo…njia ya kutupigia kura, njia kuna njia tatu. Njia ya kwanza ni kwa SMS, andika herufi AD5 kisha unatuma kwenda namba 15440. Njia ya pili unaenda kwenye Website za Kilimanjaro ambazo ni www.kilitime.co.tz utakuta kuna wimbo bora wa reggae unatupigia kura. Na njia ya tatu ni njia ya Email, ambayo ni ktma@audiotaxinternational.co.tz”
No comments:
Post a Comment