MWISHONI mwa wiki iliripotiwa juu ya msanii Shetta kupata ajali mbaya
ya gari wakati akielekea Babati, mkoani Manyara kwa ajili ya kazi za
muziki ingawa aliweza kunusurika katika ajali hiyo.
Akizungumza na Pro-24 msanii huyo alielezea kisa kizima kilichopelekea
kutokea kwa ajali hiyo mkoani huko ambapo ilisababisha kazi hiyo ya
muziki kushindwa kufanyika mkoani hapo.
Alisema kuwa chanzo cha ajali hiyo ilikuwa ni kumkwepa Pundamilia
aliyekuwa akikatiza barabarani hali iliyopelekea kpata ajali mbaya
ingawa anamshukuru mungu kuwa hivi sasa yupo salama.
"Nilitumia usafiri wa ndege kutoka Dar es Salaam, hadi Arusha ambapo
nilikuwa na kazi huko Babati kufika sehemu inayoitwa Minjingo ambapo
sehemu hiyo inakuwa na wanyama wengi kidogo , tulikutana na Pundamilia
mmoja barabarani alikuwa ameshavuka sasa wakati gari pia haijavuka nae
alikuwa anataka kurudi tena huko halafu gari lilikuwa kwenye mwendo kasi
kidogo" alisema Sheta.
Sheta ameeleza kuwa gari limeumia sana lakini wao wamenusurika ingawa
bado anamaumivu ya kawaida ambapo hivi sasa yupo hospitali kwa ajili ya
kupima afya yake kama anamaumivu yoyote ndani .
Ameweka wazi kuwa kutokana na ajali hiyo imebidi show yake iahirishwe
kwa kuwa kila mtu alikuwa amepata taarifa kuhusu ajali hiyo hivyo hakuwa
na sababu yoyote ya kuendelea na show hiyo zaidi ya kuimarisha afya
yake kwanza.
No comments:
Post a Comment