Msanii
Diamond Platnumz, ameendelea kuchana mawimbi katika anga la muziki
hususan kwa upande wa Afrika ambapo amefanikiwa kuingia katika orodha ya
wasanii 20 Bora ambao wanafanya vizuri Afrika, ambao wataingia katika
kinyanganyiro cha kuwania tuzo za Kora.
Diamond
katika orodha hii, anatokea sambamba na majina ya wasanii wakubwa
Afrika, kama vile Oliver Mtukudzi, Fally Ipupa, Mafikizolo pamoja na
wakali wengine wa muziki barani Afrika.
Kutokea
kwa Diamond katika orodha hii, ni nafasi nyingine kubwa ya kuipeperusha
bendera ya Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla, katika jukwaa la
kimataifa.
Kwa
sasa mchakato unaendelea kupitia ukurasa wa facebook wa Tuzo hizi,
ambapo maoni mbalimbali ya mashabiki yanakushanywa kuhusiana na wasanii
gani wanaokubalika zaidi, tayari kwa kuwapambaniza katika tuzo hizo
kubwa.
No comments:
Post a Comment