Kesi ya Chris Brown inaanza kuwatia wasiwasi mashabiki wake kuwa huenda hali ikawa mbaya kwa muimbaji huyo baada ya mlinzi (bodyguard) wake kukutwa na hatia katika kesi iliyomkabili ya kumshambulia mtu akiwa na Chris Brown.
Jaji Patricia Wynn ambaye anaendesha kesi ya mlinzi huyo na ya Chris Brown amesema mlinzi huyo amekutwa na hatia kutokana na ushahidi uliotolewa na dereva.
Dereva huyo ameeleza mahakamani hapo kuwa Chris Brown alimpiga Adams na baadae mlinzi wake akaingilia na kumshambulia pia. Jaji ameeleza kuwa kitendo cha mlinzi huyo hakikuwa sahihi kwa kuwa hakuna ushahidi wowote unaoonesha kuwa kijana huyo alikuwa amemsogelea Chris Brown.
Mwanafunzi mwingine wa Howard University, Jalen Garrison aliongeza kuwa yeye na rafiki yake walikuwa wanapiga picha na Chris Brown wakati ambapo Adams ambaye ni boyfriend wake alijaribu kupiga picha na mkali huyo wa With You. Lakini Chris Brown aliwaka na kumtolea maneno ya lugha chafu kabla hajampiga usoni.
Adhabu ya mlinzi huyo imepangwa kutolewa June, 25. Mlinzi huyo alikiri kuwa alimpiga mtu huyo na alijitetea kuwa alimpiga kwa nia ya kumlinda Chris Brown.
Chris Brown pia amepangwa kusimama kizimbani Jumatano, April 23 kwa kesi hiyo
No comments:
Post a Comment