Tuesday, 15 April 2014

JOTI AFUNGUKA KUHUSU MAIGIZO


              Lucas mhuvile
Mchekeshaji mahiri katika tasnia ya filamu Bongo Lucas Mhuvile ‘Joti’ amesifia kurudi kwa kundi la Kaole na kufanikiwa kutengeneza tamthilia kali nay a kusisimua ya Kipusa, Joti amedai kuwa wasanii walitoka na kufanikiwa kwa sababu walimudu katika maigizo na si katika filamu.

“Nimefurahi sana hasa kwa Kipemba kunialika na kuona kazi yenye ubora mkubwa sana, niseme ukweli huku ndio kwetu, sisi wenyewe tumetoka katika maigizo na tulifanya vizuri, katika filamu bado ndio maana hazifanyi vizuri nje ya nchi,”alisisitiza Joti.
             ZE COMEDY 538
Joti amewaomba wasanii walitoka katika makundi ya maigizo kurudi huko na kutengeneza tamthilia zitakazoelezea maisha halisi ya Watanzania kama ilivyokuwa hapo awali , kama yaliyokuwa na ushindani kama Nyota Nsemble, Kidedea, Splendid sanaa itarudi na kufanya vizuri
KWA HISANI YA FC

No comments:

Post a Comment