Kwa mujibu wa gazeti la Daily Star, chanzo kimoja kimeeleza kuwa Drake amemnunulia Rihanna zawadi ya pete ya almasi yenye rangi ya njano yenye thamani ya $42,000 (sawa na 68,712,000/-).
Hata hivyo imeelezwa kuwa pete hiyo sio ya uchumba.
“Rihanna aliikubali zawadi hiyo kama ishara ya mapenzi ya Drake. Sasa hivi (Drake) anabadili hata ratiba zake ili atumie muda mwingi ipasavyo kuwa na Rihanna.” Kilieleza chanzo hicho.
Drake na Rihanna wanaonekana kuwa karibu zaidi kadiri siku zinavyozidi kwenda, na hata Jumapili katika MTV Movie Awards walionekana wakiwa wameshikana mikono muda mfupi baada ya Drake kuperform.
No comments:
Post a Comment