Tuesday, 15 April 2014

DUDE ASEMA "BONGO MOVIE HAKUNA UPENDO"


             Kulwa Kikumba 532 b
Kulwa Kikumba ‘Dude’ Mtayarishaji na muongozaji wa filamu Bongo amewashukia wasanii wa filamu maarufu kama Bongo Movie kuwa hawana upendo wala utu zaidi ya kuangalia maslahi yao au njia ya kutengeneza fedha tu lakini siyo kutoa misaada ya kweli kwa jamii na wazazi wa wasanii waliofariki.

“Bongo Movie kumetoa taswira mbaya katika tasnia ya filamu, Visasi, chuki, ubinafsi, ugomvi, ndivyo vilivyotawala huku ubora wa filamu ukiwa umeporomoka kama si kushuka kupita kiasi hakuna ubunifu,”
“Sharo, Kanumba na Sajuki tumewasahau hakuna anayewakumbuka, kama leo mama Kanumba kaamua kuigiza usishangae mama Sharo naye akiingia kuigiza ili maisha yaende,”anasema Dude.

Dude anasema kuwa ipo haja ya kuangalia na kuiokoa tasnia ya filamu inayoekea kuzama katika kwa kasi kama vile katika mkondo hatari wa Bahari Nugwi

No comments:

Post a Comment