by rahim kassonga
JUMANNE-ARSENAL v NAPOLI, CELTIC v BARCA, STEAU v CHELSEA!
Mechi za Makundi-Raundi ya Pili:
Jumanne 1 Oktoba 2013
FC Basel 1893 v FC Schalke 04
FC Steaua BucureÅŸti v Chelsea FC
Borussia Dortmund v Olympique de Marseille
Arsenal FC v SSC Napoli
Football Club Zenit v FK Austria Wien
FC Porto Club v Atlético de Madrid
AFC Ajax v AC Milan
Celtic FC v FC Barcelona
ZIFUATAZO NI DONDOO MUHIMU ZA KILA
MECHI HIZO:
KUNDI E (FC Basel v FC Schalke 04;
FC Steaua BucureÅŸti v Chelsea FC)
• Basel na Schalke zilikutana UEFA CUP Msimu wa 2004/05 hatua za
Makundi na kutoka 1-1.
• Msimu uliopita, Steaua waliifunga Chelsea kwenye UEFA EUROPA
LIGI Raundi ya Mtoano ya Timu 16 kwa Bao la Penati ya Raul Rusescu lakini
kwenye Marudiano huko Stamford Bridge, Steau ilichapwa Bao 3-1 kwa Bao za Juan
Mata, John Terry na Fernando Torres huku Bao pekee la Steau likifungwa na Vlad
ChiricheÅŸ.
KUNDI F (Borussia Dortmund v
Olympique de Marseille; Arsenal v Napoli)
• Dortmund na Marseille zilicheza kwenye Kundi moja la UCL Miaka
miwili iliyopita na Marseille kushinda 3-0 Nyumbani na 3-2 Ugenini.
• Mara ya mwisho kwa Arsenal kucheza na Timu ya Serie A ilitolewa
nje ya UCL kwenye Raundi ya Mtoano ya Timu 16 kwa kuchapwa 4-0 na AC Milan huko
San Siro Msimu wa 2011/12 na wao kushinda 3-0 Uwanjani kwao Emirates.
KUNDI G (FC Zenit v FK Austria
Wien; FC Porto v Club Atlético de Madrid)
• Hii ni mara ya tatu kwa Zenit kucheza na Klabu za Nchini Austria
na mara ya kwanza walicheza na ASKÖ Pasching ambayo baadae ilibadilishwa Jina
na kuitwa SK Austria Kärnten na hiyo ilikuwa kwenye Misimu ya 2004/05 na
2005/06.
• Msimu uliopita Porto, walishinda Mechi zao zote za Nyumbani
kwenye UCL kwa kufunga Bao 8 na kufungwa 2 tu.
KUNDI H (AFC Ajax v AC Milan;
Celtic FC v FC Barcelona)
• Ajax walitwaa Pointi 4 kwenye Mechi za Mkundi za UCL za Msimu wa
2010/11 dhidi ya AC Milan. Wakati huo, katika Mechi ya kwanza, Zlatan
Ibrahimović aliifungia Bao AC Milan dhidi ya Ajax ambayo ilikuwa Timu yake ya
zamani na Mounir El Hamdaoui kuisawazishia Ajax na kutoka 1-1 lakini katika
Mechi ya Marudiano Ajax walishinda 2-0 kwa Bao za Demy de Zeeuw na Toby
Alderweireld.
• Rekodi ya Barcelona dhidi ya Klabu za Scotland kwa Mechi za
Nchini Scotland ni Ushindi 2 Sare 1 na Kufungwa 3.
MATOKEO-Mechi za Kwanza:
Jumatano 18 Sep 2013
FC Schalke 3 FC Steaua BucureÅŸti 0
Chelsea 1 FC Basel 2
Olympique de Marseille 1 Arsenal 2
SSC Napoli 2 Borussia Dortmund 1
FK Austria Wien 0 FC Porto 1
Club Atlético de Madrid 3 Football Club Zenit 1
AC Milan 2 Celtic FC 0
FC Barcelona 4 AFC Ajax 0