Mario
Balotelli amefungiwa Mechi 3 kwa kutumia ‘vitisho na matusi’ dhidi ya Refa mara
baada ya Mechi ya Serie A Juzi ambayo Timu yake AC Milan ilichapwa Bao 2-1 na
Napoli Uwanja wa kwao San Siro.
Balotelli
alitolewa kwa Kadi Nyekundu baada ya Mechi hiyo kwisha kufuatia kupewa Kadi ya
Njano ya Pili baada ya yeye kuvaana na Mchezaji wa Napoli Valon Behrami na
kisha kuanza kukwaruzana na Refa Luca Banti.
Katika
Mechi hiyo, Balotelli alikosa Penati iliyookolewa na Kipa wa Napoli, Pepe
Reina, na baadae kupiga shuti lililogonga mwamba na Dakika za mwisho kuifungia
AC Milan hilo Bao lao moja kwa Shuti murua.
Hiyo
ilikuwa ni mara ya kwanza kabisa kwa Balotelli kukosa Penati tangu aanze Soka
la Kulipwa.
AC Milan
haijasema lolote kama itakata Rufaa kupinga Kifungo hicho na kama kitabaki kama
kilivyo basi Balotelli atazikosa Mechi za Serie A dhidi ya Bologna, Sampdoria
na Juventus.
Wakati
huon huo, Wasimamizi wa Soka huko Italy wameamuru AC Milan kufunga Jukwaa lao
la Uwanja wa San Siro linaloitwa Curva Sud kwenye Mechi ijayo na Sampdoria kama
Adhabu kwa Mashabiki waliokuwa wakighani Kibaguzi wakati wa Mechi waliyofungwa
na Napoli.
No comments:
Post a Comment