Messi Lionel alitolewa baada ya kuumia mguu wakati Barcelona ikiwapiga Almeria 2-0 huku akiweka rekodi ya klabu hiyo kushinda michezo saba mfululizo ya ligi mwanzoni mwa msimu
Muargentina huyo , ambaye alifunga goli lake la nane kwenye ligi msimu huu anatarajiwa kufanyiwa vipimo jumanne wiki hii
Mbrazil Adriano ndiye aliyeipatia Barca bao la pili 'baada ya mapumziko baada ya kuunganisha krosi hafifu ya Fabrigas.
Messi, 26, ambaye alionekana mbele ya hakimu wa Kihispania ijumaa katika kesi inayomkabilia ya udanganyifu
wa kodi aliiwezesha Barcelona kuongoza katika dakika ya 21, alipopiga shuti kali umbali wa yadi 20, lakini dakika nane
baadae alitolewa baada ya kuumia
Gerardo Martino, ambaye aliteuliwa kuwa kocha wa Barca katika majira ya joto, amezishinda rekodi zilizowekwa na mameneja wengine watano waliomtangulia akiwemo - Pep Guardiola (2009-10) na Tito Vilanova (2012-13) ambao
walifanikiwa kuanza kwa kushinda michezo 6 mfululizo
Lakini taarifa toka ndani ya klabu hiyo zinasema mchezaji huyo atakaa nje kwa wiki 2 hadi 3
No comments:
Post a Comment