by rahim kassonga
KILIMANJARO
Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetangaza operesheni maalumu ya kumuondoa
Mbunge wa Jimbo la Same Magharibi Dk
David Mathayo David katika Uchanguzi Mkuu wa 2015.
Operesheni hiyo imepewa
jina la Operesheni Mathayo Out kwa kifupi (OMO) imeanza wiki iliyopita kwa
kufanya Mikutano ya hadhara Jimboni humo na itaendelea tena wiki ijayo.
Aidha Mmoja wa Makamanda
wa Operesheni hiyo Gervas Mgonja amesema
kuwa Jimbo hilo limekuwa chini ya himaya ya CCM tangu Uhuru lakini wananchi
wake wapo kama wamefunga ndoa na tatizo la maji.
Dk Mathayo
ambaye pia ni Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi alipoulizwa kuhusu
operesheni hiyo ya kumuondoa madarakani amesema kuwa Chadema ni chama kidogo na
hakimnyi usingizi kwa madai uwezo wa kampeni unaishia Himo.
EDITOR:TIDA SAIDEA
No comments:
Post a Comment