Friday, 20 September 2013

LIGI KUU ULAYA KUENDELEA WIKIENDI



by rahim
JUMAPILI NI MANCHESTER DABI!
BAADA kuburudishwa na Mashindano makubwa ya Vilabu Barani Ulaya, Wapenzi wa Soka la England Wikiendi hii watashuhudia michuano mbalimbali ya soka katika ligi za ulaya zikiendelea wikiendi hii
Kipute cha ligi za ulaya kinaanzia leo ambapo
France - Ligue 1 September 20
21:30
Saint Etienne
? - ?
Toulouse


Germany - Bundesliga September 20
21:30
Borussia Monchengladbach
? - ?
Braunschweig


Spain - Liga BBVA September 20
22:00
Osasuna
? - ?
Elche
Ligi hizo zitaendelea tena jumamosi katika viwanja mbalimbali ambapo

14:45
Norwich City
? - ?
Aston Villa
17:00
Liverpool
? - ?
Southampton
17:00
Newcastle United
? - ?
Hull City
17:00
West Bromwich Albion
? - ?
Sunderland
17:00
West Ham United
? - ?
Everton
19:30
Chelsea
? - ?
Fulham
SERIE A
Napoli, ambao ndio Vinara wakiwa na Pointi 9 kwa kushinda Mechi zao zote 3, wako Ugenini kucheza na AC Milan walio Nafasi ya 9 na wana Pointi 4.
Timu ya Pili ambayo inafungana kwa Pointi na Napoli ni AS Roma ambao watakuwa Nyumbani kucheza na Lazio ambao wako Nafasi ya 7 na wana Pointi 6.
Mabingwa Watetezi, Juventus, wambao wako Nafasi ya 4, Pointi 2 nyuma ya Vinara, wako Nyumbani kucheza na Hellas Verona, Timu iliyopanda Daraja Msimu huu.


19:00
Cagliari
? - ?
Sampdoria
19:00
ChievoVerona
? - ?
Udinese
21:45
Genoa
? - ?
Livorno

Barcelona watakuwa wakiwania rekodi yao ya kushinda Mechi zote za Ligi Msimu huu watakapokwenda Ugenini kucheza na Rayo Vallecano.
Barca wana Pointi 12 kwa Mechi 4 na wanakutana na Rayo ambayo imepakia Bao 12 katika Mechi zao 3 za mwisho.
Mara ya mwisho Barca kwenda Nyumbani kwa Rayo, Estadio de Vallecas Teresa Rivero, waliichapa Rayo Bao 5-0 Msimu uliopita na 7-0 Msimu wa 2011/12 na hawajafungwa na Timu hiyo tangu Desemba 2002.
Real Madrid, ambao wako Pointi 2 nyuma ya Barca, wapo Nyumbani Santiago Bernabeu kucheza na Getafe na hii ni Mechi inayofuatia Sare ya 2-2 na Villareal Wikiendi iliyopita.
Lakini, Real wanaingia kwenye Mechi hii wakiwa na moto baada ya kuifumua Galatasaray Bao 6-1 huko Uturuki Siku ya Jumanne kwenye Mechi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI huku Cristiano Ronaldo akipiga Bao 3.
Msimu uliopita Getafe, ikiwa Nyumbani, iliifunga Real lakini katika Mechi 3 za mwisho kwenda Bernabeu wamekuwa wakibebeshwa Bao 4 kila Mechi.
Timu pekee nnyingine ambayo imeshinda Mechi zote za Ligi Msimu huu ni Atletico Madrid ambayo ina Pointi sawa na Barca na watakuwa Ugenini kucheza na Real Valladolid.


17:00
Real Sociedad
? - ?
Malaga
19:00
Almeria
? - ?
Levante
21:00
Rayo Vallecano
? - ?
Barcelona
23:00
Valladolid
? - ?
Atletico Madrid

BUNDESLIGA
Kikosi cha Jurgen Klopp, Borussia Dortmund,  kimeshinda Mechi zao zote 5 Msimu huu na kufunga Bao 15 na kufungwa 4 tu, na ingawa Juzi kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI kilichapwa Ugenini na Napoli huku Klopp na Kipa wao Roman Weidenfeller, wakitolewa nje kwa Kadi Nyekundu.
Dortmund, ambao Wikiendi iliyopita waliibamiza Hamburg Bao 6-2 kwenye Bundesliga, watacheza Ugenini na Nurnberg.
Mabingwa Watetezi, Bayern Munich, ambao wako Pointi 2 nyuma ya Dortmund, wako Ugenini kucheza na Schalke.
16:30
Hamburger SV
? - ?
Werder Bremen
16:30
Hannover 96
? - ?
Augsburg
16:30
Mainz 05
? - ?
Bayer Leverkusen
16:30
Nurnberg
? - ?
Borussia Dortmund
16:30
Wolfsburg
? - ?
Hoffenheim
19:30
Schalke 04
? - ?
Bayern Munich



18:00
Bastia
? - ?
Marseille
21:00
Evian Thonon Gaillard
? - ?
Montpellier
21:00
Reims
? - ?
Guingamp
21:00
Rennes
? - ?
Ajaccio
21:00
Sochaux
? - ?
Lille
Mechi hizo zinatarajiwa kuendelea tena jumapili, wakati kutakuwa na mechi yenye mvuto zaidi ni kati ya Manchester City wazee wa jiji wakiwakaribisha Manchester United kwenye uwanja wa Etihad
Hadi sasa Liverpool ndio wako kileleni wakiwa na Pointi 10 baada kushinda Mechi 3, ikiwemo kuwafunga Mabingwa Watetezi Manchester United Bao 1-0, na kutoka Sare moja.
Nyuma ya Liverpool zipo Arsenal na Tottenham zinazofungana kwa Pointi, zote zikiwa na 9, na kisha zinafuata Timu 5 zenye Pointi 7 kila moja na hizo ni Man City, Man United, Chelsea, Stoke City na Newcastle.
Kuhusu dabi tukutane kesho kuanzia saa 12 hadi saa 3 asubuhi
8888888888888888888888888888888888888888888888888888
LIGI KUU ENGLAND: KLABU, WACHEZAJI KUAMUA KUVAA NYUZI ZA ‘USHOGA’!!

WACHEZAJI Soka huko England na Scotland wamealikwa kuisaidia Kampeni ya kuunga mkono Mashoga kwa kutakiwa kufunga Nyuzi za Rangi ya ‘Upinde wa Mvua’ kwenye Buti za0 wakati wa Mechi za Wikiendi hii
WASIMAMIZI wa LIGI KUU ENGLAND wamesema ni juu ya Klabu zenyewe na Wachezaji wenyewe kuamua kama wataunga mkono Kampeni ya Kutetea Haki za Mashoga kwa kufunga Nyuzi za Rangi ya ‘Upinde wa Mvua’ kwenye viatu vyao wakati wa Mechi za Ligi za Wikiendi hii.
Tayari Taasisi ya Hisani ya Mashoga, ya Stonewall, imetuma Nyuzi hizo spesho kwa Vilabu 92 vya Ligi Kuu England na Klabu za Ligi za Madaraja ya chini na pia Klabu 42 za Soka ya Kulipwa huko Scotland.
Kwenye Kampeni hii, iitwayo The Right Behind Gay Footballers, Wachezaji wataombwa kutumia Nyuzi hizo kwenye Mechi za Septemba 21 na 22.
Lakini Msemaji wa Ligi Kuu England amesema: “Ujumbe wa msingi wa Kampeni hii ni mzuri na ni kweli sisi na Wadau wetu tumeshirikiana na Serikali kuhakikisha Ajenda yote ya Usawa inaeleweka na tunashiriki. Lakini hatukuhusishwa mapema kwenye Kampeni hii. Hivyo ni juu ya Klabu na Wachezaji wenyewe kuamua kama wanaisapoti.”
Lakini Klabu nyingi zimeonyesha kutoridhishwa kwao kwa jinsi Kampeni hiyo inavyoendeshwa na Taasisi ya Hisani ya Mashoga, Stonewall, na Kampuni ya Kamari, Paddy Powers, bila ya wao kuhusishwa tangu awali.
BAADHI ya Klabu za Ligi Kuu England, zikiwemo Mabingwa Manchester United, Tottenham na Norwich City, zimegoma kutoa sapoti kwenye Kampeni ya Kutetea Haki za Ushoga.
Tamko rasmi la Mabingwa Manchester United limesema Klabu hiyo haitavaa Nyuzi hizo huku nao Tottenham wakiwa na msimamo huo huo pamoja na Norwich ambao Meneja wao Chris Hughton amesema Wachezaji wake hawatavaa Nyuzi hizo.

Huku klabu zingine zote zilizosalia zimeonesha kukubaliana na wazo hilo
Huko Uingereza, haki za Mashoga zinalindwa na hata FA ina msimamo wa kukemea Mashoga kubaguliwa.
Kwa sasa hakuna hata Mchezaji mmoja huko Uingereza alieibuka bayana na kukiri yeye ni Shoga.
Mwaka 1990, Mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa ya England na U-21 , Justin Fashanu, alikuwa ni Mchezaji wa kwanza wa Kulipwa kutangaza yeye ni Shoga lakini Mwaka 1998, Fashanu alijiua mwenyewe akiwa na Miaka 37.

No comments:

Post a Comment