Kutokana kuwa majeruhi, mcheza kikapu nyota wa timu ya Los
Angeles Lakers Kobe Bryant anaweza kusogezewa muda wa kurudi tena uwanjani
mpaka atakapokuwa sawa
Hali hiyo imemfanya asionekane katika michezo ya kujiandaa
na ligi hiyo maarufu kama pre season
Kobe Bryant - nyota w NBA na Los
Angeles Lakers,
Imeripotiwa
kuwa Bryant amebakiwa wiki chache kabla ya kuwa fiti 100% kwa kuanza mazoezi
mepesi yeye mwenyewe
Aliumia
mwezi April na kuwa fiti kabisa itamchukua miezi sita hadi 8
Timu
ya Lakers ilitangaza kumsajili Ryan Kelly kuziba nafasi ya Kobe kwenye kipindi
hiki kigumu
Kelly
amechukuliwa na Lakers mwezi june kwenye awamu ya pili ya michuano ya vyuo
nchini marekani ambapo alikua kwenye Chuo kikuu cha Duke.
Wakati
huo alikuwa na wastani wa pointi 12.9 na reboundi 5.3 na blocked short 1.6
Nae
mlinzi wa Brooklyn Nets Deron Williams alipoongea na vyombo vya habari mjini
New York amesema atakuwa sawa kuanza mazoezi nakuingia kwenye kambi mwezi
October mwaka huu japokuwa vipimo vya
sumaku vinaonesha kuwa anatatizo la enka kwenye mguu wake wa kulia
Williams,
ambaye alisema tatizo hilo la enka ameumia alipokuwa na Utah Jazz wiki mbili
zilizopita alipokuwa akitembea na kupata tatizo linalojulikana kitaalam kama bone bruise
No comments:
Post a Comment