Tuesday, 24 September 2013

TANZANIA YATWAA UBINGWA AIRTEL RISING STARS WANAWAKE, YATOA PIA WACHEZAJI BORA

by rahim kassonga



TIMU ya wasichana ya Tanzania imeibuka mabigwa katika michuano ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya kimataifa ya Airtel Rising Stars yaliyokuwa yanafanyika mwaka huu nchini Nigeria, baada ya kuifunga Kenya bao 1-0 katika Fainali. 




Donisia Daniel ndio alipeleka furaha kwa upande wa Tanzania kwa kufunga bao hilo pekee la ushindi jana.
Tanzania ilikua kundi moja na Sierra-Leone, Malawi, na Uganda. Walishinda mechi moja dhidi ya Sierra-Leone 2-1, wakapoteza mchezo dhidi ya Uganda na kutoka sare na Malawi 1-1.



Katika Robo Fainali, mabinti wa kibongo wakashinda 4-2 kwa mikwaju ya penalti dhidi ya DRC Uwanja wa NIS Sports, kabla ya kuifumua Uganda kwa mabai 8-1 kwenye Nusu Fainali.
Mbali na ushindi huo wa wasichana wa Tanzania walijishindia zawadi mbalimbali ikiwemo , Mchezaji bora kwa upande wa wasichana Tatu Iddi, Mfungaji bora wa mashindano kwa upande wa wavulana Athanas Mdam na Mfungaji bora kwa upande wa wasichana Shelda Boniface.
Kwa upande wa wavulana Timu ya Niger wametetea tena ubingwa  baada ya kuifunga Zambia kwa mikwaju ya penati 7-6  katika mechi ya fainali ya Airtel Rising Stars ilifanyika kweny uwanja wa Agege nchini Nigeria.










Niger wamefanya vizuri kuanzia hatua ya makundi  baada ya kushinda michezo yote katika makundi na kufikisha magoli 12 na kuruhusu magili matatu tu katika mechi sita. Jumla ya mechi 58 zimechezwa katika mashinda.
Aidha timu ya wavulana ya Tanzania imeshikilia nafasi ya nne kati ya timu zaidi ya 16 zilizoshiriki michuano hiyo
Michuano ya kimataifa ya Airtel Rising Stars kwa mwaka huu yamefanyika nchini Nigeria katika viwanja vinne Agege, Township Stadium, Legacy Pitch, National Institute for Sports Fiels na Main Bowl.
Mashindano ya kiamataifa ya umri chini ya miaka 17 ya Airtel Rising Stars yanafanyika kwa mara ya pili mwaka huu na yamekua bora kwa vijana wadogo na kwa kuzingatia jinsia.

No comments:

Post a Comment