Friday, 29 August 2014

MCHUNGAJI AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUISHI NA MKE WA MUUMINI WAKE




Pichani ni Mchungaji, Israel Mwakifuna, wa Kanisa la Jeshi la Bwana(JB)lililopo Nzovwe jijini Mbeya 
KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, ambapo wananchi wengi wanaamini Mchungaji ni sehemu ya kukimbilia kueleza matatizo yao hususani migogoro ya kindoa, hali imekuwa tofauti jijini Mbeya.
Utata umeibuka baada ya Mchungaji, Israel Mwakifuna, wa Kanisa la Jeshi la Bwana(JB)lililopo Nzovwe jijini Mbeya amefikishwa katika Mahakama ya mwanzo ya Iyunga jijini Mbeya akituhumiwa  kuishi na mke wa mtu ambaye ni muumini wake.
Mchungaji huyo alifikishwa juzi mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Iyunga, Nuru Lyimo akisaidiwa na Washauri wa mahakama Edson Mbeba na Rehema Haonga.
Kesi hiyo ya madai namba 51/2014 imepelekwa mahakamani hapo na  William Daimon Mwasubila(23)mkazi wa Nzovwe ambapo imedaiwa mahakamani Mchungaji kuishi na mke wake aitwaye Helena Mkea(21) kwa muda wa miezi minne sasa.
Mlalamikaji katika Kesi hiyo, Mwasubila aliiambia mahakama kuwa alikuwa akiishi na mkewe bila tatizo lakini matatizo yalianza pindi mkewe aliposhika ujauzito na kuamua kwenda kwa wakwe zake kwa matazamio baada ya mapishano yaliyodhaniwa kusababishwa na ujauzito hali ambayo alikubali.
Mwasubila alieendelea kuiambia mahakama kuwa mkewe alimuoa kihalali kupitia mshenga wake aliyefahamika kwa jina la Edward Mwangoje ambapo walifuata taratibu zote za mila kwa kulipa kiingilio cha mlangoni 50,000,kufungua 20,000,adhabu 50,000, kuku wawili, mashuka, mablanketi mawili na majembe mawili.
Alivitaja vitu vingine alivyolipia kama mahali kuwa ni mkaja wa mama 150,000 ambapo alilipa elfu hamsini,Mbuzi wawili jike na dume,n'gombe watatu dume ambao kila mmoja akiwa na thamani ya shilingi 300,000 na kupokelewa na wazazi kupitia kwa mshenga Octoba 20 mwaka 2013 eneo la Airport Jijini Mbeya.
Alisema mgogoro katika ndoa yao ulianza baada ya Mume kuzikuta SMS za mapenzi kwenye simu ya mkewe kwenda kwa mchungaji Mwakifuna ambapo alitoa taarifa kwa wazazi wapande zote mbili ambapo walijadili na kuondoa tofauti hizo na kuamua kuwasamehe.
Aliongeza kuwa  muda mfupi baada ya mazungumzo Mchungaji aliendelea kuwa na mahusiano ya kimapenzi na muumini wake hali iliyosababisha mke wa mchungaji Mwakifuna kuondoka kwa mumewe miezi minne iliyopita baada ya yeye(Mlalamikaji) kwenda kikazi Sumbawanga Mkoani Rukwa ambapo mkewe alihamia kwa Mchungaji wake na kuanza kuishi kama mke na mume.
Aliendelea kuiambia Mahakama kuwa Baada ya kutoka Sumabwanga  alipata taarifa kuwa mkewe anaishi na mchungaji ambapo aliamua kutoa taarifa Polisi kituo cha Nzovwe.
Alisema Jeshi la Polisi lilifika nyumbani kwa Mchungaji na Kumkuta  mkewe akiwa na mtoto wake wa kike mwenye umri wa wiki moja na nusu ndipo alipokamatwa  Agosti 25 na kufikishwa mahakamani Agosti 26, mwaka huu.
Baada ya kusikiliza shahidi mmoja wa upande wa mlalamikaji Hakimu Lyimo aliiahirisha kesi hiyo hadi Septemba 3, mwaka huu mlalamikaji atakapoleta mashahidi wengine kwa ajili ya kutoa ushahidi wao.

SABBY: RUSHWA YA NGONO BONGO MUVI IMENITESA


Msanii wa filamu, Salma Omary ‘Sabby’ ameamua kufunguka kuwa ameteswa sana na rushwa ya ngono aliyokuwa akikutana nayo pindi alipokuwa akifurukuta kutoka kisanii.
Msanii wa filamu, Salma Omary ‘Sabby’ akipozi.
Akizungumza  Sabby alisema, tatizo hilo la rushwa anaweza kuwa miongoni mwa wasanii waliosumbuliwa sana wakati kuna baadhi walipokuwa wakitolewa nje, walikuwa wanajenga bifu naye na wengine kumtishia kumharibia.
“Mimi kitu ambacho kinaniumiza sana mpaka leo ni jinsi wanawake tunavyodhalilishwa kila siku, naumia mno nimepita katika tabu nyingi mpaka nafikia hapa leo, ila namshukuru Mungu siku zote,” alisema Sabby ambaye ameng’ara kwenye filamu kama vile Siri ya Gining, Hard Price, Moto wa Radi, Dr. Ray na nyinginezo.

MUME WA MTU: SIMUACHI NG’O AUNT


Mcheza shoo wa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond,’ Moses Iyobo amefunguka kwa mara ya kwanza baada ya kuenea uvumi wa kutoka kimapenzi na mcheza filamu mahiri Bongo, Aunt Ezekiel kuwa hawezi kumuacha msanii huyo ng’o.
Mcheza shoo wa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond,’ Moses Iyobo (katikati).
Akizungumza  hivi karibuni, Moses alisema kuwa kutokana na maneno mengi kuenea kuwa anatoka na Aunt, ameona ni bora aweke wazi hisia zake kwamba ni kweli anampenda msanii huyo na kuwa naye mbali itakuwa vigumu.
Mcheza filamu mahiri Bongo, Aunt Ezekiel.
“Mengi yameongelewa sana sasa naweka wazi kuwa nampenda sana Aunt. Unajua kama mtu haukuwa na uhusiano naye mara unaanza kusikia vitu vya ajabu bora tu ufanye kweli hata kama wanakusema wakuseme kihalali na si vitu ambavyo si vya kweli,” alisema dansa huyo ambaye ni mume wa mwanamke aliyefahamika kwa jina moja la Mwegi.

SHEMEJI WA WEMA ATANGAZA NDOA NA DADA WA DIAMOND


MAPENZI bwana! Baada ya kuogelea kwa muda mrefu katika penzi la muigizaji Kajala Masanja, hatimaye shemeji wa aliyekuwa rafiki wa mwigizaji huyo, Wema Sepetu, Ahmed Hashimu ‘Petit Man’ ametangaza ndoa na dada wa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Esma Abdul.
Dada wa Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Esma Abdul akila ujana na Ahmed Hashimu 'Petit Man'.
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini kilicho karibu na Diamond na Wema ambao penzi lao lilipata ‘mushkeli’ kidogo hivi karibuni, Petit Man tayari ameshakamilisha kila kitu kinachotakiwa kufanyika kabla ya ndoa na kilichobaki ni kutamka siku husika tu.
Kilidai kuwa, Petit alichukua uamuzi huo baada ya kushauriwa na Wema kuwa umri unakwenda na vishawishi ni vingi hivyo ni bora aoe mapema.“Unajua Petit Man anamheshimu sana Wema kwa hiyo alipomwambia Petit kuwa umri unazidi kwenda na anahitaji kuwa na familia yake akaukubali ushauri wake,” kilinyetisha chanzo hicho.
Esma Abdul akipozi.
Baada ya kupata maelezo hayo, MPANDA FM lilimtafuta Petit Man na kumuuliza kuhusiana na ishu hiyo, bila kuumauma maneno alikiri.“Ni kweli mama (Wema) aliniweka chini na kuniambia kuwa umri unakwenda hivyo nahitaji niwe na familia yangu kwa hiyo siwezi kuwa na familia bila ya kuwa na mke ndipo aliponichagulia mke ambaye ni dada yake wa damu kabisa na Nasibu Abdul ‘Diamond’ anayeitwa Esma na kwa taarifa yako tu, tayari nimeshakamilisha kila kitu,” alisema Petit.
'Petit Man' wakati akiwa na Kajala.
Alipoulizwa kuhusiana na wanawake aliowahi kuwa nao kipindi cha nyuma akiwemo Kajala, Petit alisema huko kote ilikuwa ni njia ya kuelekea kwenye kilele cha mafanikio ambayo ni ndoa yake na Esma.
“Acha nipumzike na madhira ya dunia maana huko kote nilipopita hakukuwa chaguo langu ila kwa Esma nimekufa nimeoza bado kuzikwa tu yaani mimi ni mfu ninayetembea mbele ya Esma.”

TFF YAIBEBA YANGA


jaja

Shirikisho la soka nchini, TFF limesogeza mbele muda wa usajili kwa klabu za ligi kuu na ligi daraja la kwanza kwa masaa 48 zaidi, Siku mbili kwa wachezaji wa ndani na wiki moja zaidi kwa usajili wa wachezaji wa kigeni kutoka nje ya nchini. Uamuzi huo umefikiwa baada ya klabu zote 14 za ligi kuu na 15 za ligi daraja la kwanza kushindwa kukamilisha taratibu za uhamisho wa Kieloktroniki. Ni timu moja tu iliyoweza kukamilisha usaajili wake siku ya jana ambayo ilikuwa ni ya mwisho baada ya mara mbili kuongezwa kwa muda.
Yanga SC wameshindwa kupata hati ya uhamisho wa kimataifa ( ITC) ya mshambulizi, Geilson Santos ‘ Jaja’ na kuna uwezekano mkubwa wa mchezaji huyo kutoka Brazil akaondolewa kat
ika timu hiyo. Katikati ya mwaka 2010 timu hiyo ilishindwa kukamilisha taratibu za kumuhamisha mshambulizi raia wa Ghana, Keneth Asamoah aliyekuwa akichezea klabu ya FK Jagodina ya Serbia.
Jaja anaweza kutemwa na kuwapisha Waganda, Hamis Kizza na Emmanuel Okwi kuungana na wachezaji wengine wa kimataifa, Haruna Niyonzima, Mbuyu Twite na Andry Coutinho. Jina la mchezaji halipo katika orodha ya wachezaji wa Yanga na hakuna maombi yoyote ambayo uongozi wa Yanga umewasilisha kwa shirikisho la soka nchini, TFF hadi kufikia siku ya jana. Kama mshambulizi huyo atakwama kusajiliwa kama ilivyokuwa kwa Asamoah huku akiwa na mkataba wa miaka miwili uongozi hautakwepa lawama hivyo wanatakiwa kufanya kila wawezalo na si kujiaminisha kupata msaada wa muda mrefu kutoka kwa Okwi, na Kizza.
Afadhali kwa Kizza yeye ni mchezaji wa Yanga hasa ila Okwi ataendelea kuwasumbua Yanga.
Uongozi wa Yanga unasema kuwa kumekuwa na tatizo la mawasiliano kati yao na Shirikisho la soka la Brazil, CBF, ila hawajafanya jitihada za kupeleka maombi hayo rasmi kwa TFF ambao watafanya mawasiliano na wenzao wa Brazil ili kuhakikisha mchezaji huyo anasajiliwa na kukamilisha taratibu zote.
Itakuwa ni sawa na kukosa umakini kwa viongozi wa Yanga kwa kuwa wamekuwa wakifahamu, Jaja ni mchezaji wao mpya tangu mwezi uliopita. Mfumo wa TMS umekuwa ukiwasumbua viongozi wa klabu za Tanzania lakini maombi ya uhamisho wa wachezaji yanayofanywa kutumia mfumo huo hufanyika haraka.

SaSA Yanga wamepata muda zaidi wa kufikiria kwa umakini ni mchezaji gani wa kigeni anayetakiwa kuachwa kati ya washambuliaji hao watatu. Kulikuwa na uwezekano mkubwa wa Jaja kuachwa, lakini matumaini ya Mbrazil huyo kucheza Tanzania yamerejea baada ya muda zaidi wa usajili kuongezwa.

OKWI AREJEA SIMBA SC KUCHEZA KWA MUDA KULINDA KIPAJI CHAKE WAKATI KESI YAKE NA YANGA IKIENDELEA


STAILI ile ile waliyotumia Yanga SC kumpata mshambuliaji Emmanuel Arnold Okwi ndiyo ambayo klabu yake ya zamani, Simba SC inaitumia kumrejesha kundini Mganda huyo. Akizungumza na Waandishi wa Habari jioni hii mjini Dar es Salaam, Okwi amesema kwamba amesaini Simba SC mkataba huru wa muda, baada ya Yanga SC kumpa barua ya kusitisha mkataba naye jana pamoja na kumshitaki Shirikisho la Soka Tanzania (TFF). Okwi amesema ameamua kuomba kuichezea Simba SC kipindi hiki ambacho ana matatizo na Yanga SC ili kulinda kipaji chake, kwa kuwa hata FIFA haitaki mchezaji akae bila kucheza.

“Sasa wakati Yanga wanaendelea na kesi yao, mimi ninaomba nichezee Simba SC ili kulinda kipaji changu. Nimewaandikia barua TFF na FIFA pia na nina matumaini usajili wangu utaidhinishwa, kwa sababu mimi si tatizo katika hili,”amesema. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema kwamba wamemsaini mchezaji huyo baada ya kupitia kwa kina suala lake na Yanga SC na kugundua haki ipo upande wa mchezaji. “Baada ya kulipitia suala lake na Yanga kwa undani kabisa na vielelezo ambavyo mchezaji mwenyewe ametupatia, tumejiridhisha tuko sahihi kumsaini ili acheze mpira kunusuru kipaji chake kipindi hiki ambacho ana matatizo na Yanga SC,”amesema Poppe.  
Yanga mtanikoma; Okwi akiwa ameshika jezi yake nbamba 25 kwa pamoja na Hans Poppe
Tayari Simba SC imetuma jina la mchezaji huyo katika usajili wake TFF na ataungana na Mganda mwenzake, Joseph Owino, Warundi Pierre Kwizera na Amisi Tambwe na Mkenya, Paul Kiongera katika wachezaji watano wa kigeni.   “Tumewaandikia barua TFF kuomba kumtumia mchezaji huyu kwa muda wakati kesi yake na Yanga inaendelea, tumeambatanisha na barua yake ambayo yeye anatuomba kucheza kwetu kulinda kipaji chake,”amesema Poppe. Okwi aliichezea Simba SC tangu mwaka 2009 kabla ya Januari mwaka jana kuuzwa kwa dola za Kimarekani 300,000 Etoile du Sahel ya Tunisia. Etoile haikulipa fedha hizo Simba SC na baadaye ikaingia kwenye mgogoro na Okwi, aliyedai hakulipwa pia mishahara yake kwa miezi mitatu. Okwi akawafungulia Etoile kesi FIFA na akaomba wakati mgogoro wao unaendelea, aruhusiwe kuchezea timu yoyote kulinda kipaji chake, ndipo akajiunga na SC Villa ya kwao. Akiwa SC Villa ndipo aliposaini Yanga SC Desemba mwaka jana na pamoja na mapingamizi yaliyoanzia ndani, na baadaye klabu yake, Etoile- lakini Okwi aliidhinishwa kuichezea timu hiyo ya Jangwani. Okwi aliichezea Yanga SC mechi 11 na kuifungia mabao matano- lakini kuelekea mechi tano za mwisho za Ligi Kuu msimu uliopita akaingia kwenye mgogoro na klabu hiyo. Okwi alisusa kushinikiza amaliziwe fedha zake za usajili na mgogoro wao umeendelea huku mchezaji huyo akiwa amesusa tangu Machi, miezi minne tu baadaye tangu asajiliwe. Vikao kadhaa vimekwishafanyika baina ya Okwi na Yanga SC tangu hapo kutafuta suluhu ya suala hilo na kikao cha mwisho leo baina ya mchezo huyo na Mwenyekiti wa klabu hiyo, Yussuf Manji matokeo yake ni nyota huyo kurejea Msimbazi. Kuhusu deni lao la dola 300,000 kumuuza mchezaji huyo Etoile, Poppe amesema haihusiani kabisa na usajili wake huu wa sasa. “Ile kesi yetu ya madai ya fedha zetu kule FIFA ilikwishamalizika na vielelezo vyote vilipelekwa, bado kutolewa hukumu tu,” amesema.

MAN CITY YAPEWA BAYERN MUNICH LIGI YA MABINGWA, LIVERPOOL NA REAL, CHELSEA NA WAKALI WENGINE WA UJERUMANI

MABINGWA wa England, Manchester City wamepangwa kundi moja na mabingwa wa Ujerumani, Bayern Munich katika Ligi ya Mabingwa Ulaya pamoja na CSKA Moscow na Roma, wakati Liverpool wao wamepangwa na mabingwa watetezi, Real Madrid.
Mabingwa mara tano Ulaya, Liverpool mbali na kupangwa na mabingwa mara 10 wa taji hilo, Real pia wapo na Basle na Ludogorets.
Arsenal, imepangwa na Borussia Dortmund pamoja na Galatasaray na Anderlecht katika Kundi D, wakati Chelsea imepangwa na imepangwa na wakali wengine wa Ujerumani, Schalke, Sporting Lisbon na Maribor.

KUNDI A 

Atletico Madrid 
Juventus 
Olympiakos 
Malmo 

KUNDI B 

Real Madrid 
Basle 
LIVERPOOL
Ludogorets 

KUNDI C 

Benfica 
Zenit St Petersburg 
Bayer Leverkusen 
Monaco 

KUNDI D 

ARSENAL
Borussia Dortmund 
Galatasaray 
Anderlecht 

KUNDI E 

Bayern Munich
MANCHESTER CITY
CSKA Moscow 
Roma 

KUNDI F 

Barcelona 
Paris St-Germain 
Ajax 
Apoel Nicosia 

KUNDI G 

CHELSEA
Schalke 
Sporting Lisbon 
Maribor 

KUNDI H 

Porto 
Shakhtar Donetsk 
Athletic Bilbao 
Bate Borisov 
Mkali wao: Cristiano Ronaldo akiwasili kwenye drop ya Ligi ya Mabingwa Ulaya leo mjini Monaco, Ufaransa

RONALDO ALIVYOSHEREHEKEA TUZO YAKE YA UFALME WA SOKA ULAYA LEO UFARANSA



Busu kwenye tuzo: Nyota wa Ureno na Real Madrid, Cristiano Ronaldo akibusu tuzo yake ya Mwanasoka Bora wa Ulaya baada ya kukabidhiwa usiku wa leo mjini Monaco, Ufaransa
Cristiano Ronaldo akifurahia na tuzo yake
Ronaldo (katikati) akifurahia baada ya kushinda. kushoto ni wachezaji wa Bayern Munich, kipa Mjerumani Manuel Neuer na winga Mholanzi Arjen Robbe kulia

UNYAMA;MTOTO ABAKWA NA KUUAWA KINYAMA HUKO SHINYANGA


 
Mazishi ya mwanafunzi aliyeuawa kikatili kwa kubakwa kisha kutobolewa macho na watu wasiofahamika kisha mwili wake kutupwa kichakani katika kijiji cha Nhelegani kata ya Kizumbi katika manispaa ya Shinyanga yamefanyika katika makaburi ya familia katika kijiji cha Negezi kata ya Mwawaza katika manispaa ya Shinyanga.

Mwanafunzi huyo  aliyekuwa anasoma darasa la tatu katika shule ya Msingi Negezi iliyopo kata ya Mwawaza manispaa ya Shinyanga alikutwa ameuawa kwa kubakwa kisha kutobolewa Agosti 25 mwaka huu saa saba mchana katika kitongoji cha Kashampa kijiji cha Nhelegani kata ya Kizumbi.


Akizungumza wakati wa mazishi ya mwili wa marehemu  yaliyofanyika JANA MCHANA naibu meya wa manispaa ya Shinyanga David Nkulila alilaani kitendo cha kinyama alichofanyiwa mtoto huyo huku akiitaka jamii kushirikiana na jeshi la polisi katika kuwafichua wahusika wa mauaji hayo.

“Kifo cha mtoto huyu ni mapenzi ya mungu yaliyosababishwa na wanadamu wabaya,naomba suala la hili lifuatiliwe hatuhitaji siasa katika hili inauma sana kwani vitendo vya ukatili dhidi ya watoto vinatishia amani Shinyanga”,alieleza Nkulila.

 Kwa upande wake Intelijensia mkoa wa Shinyanga Bundala Maige alisema suala la ulinzi kwa watoto ni jamii nzima na kwamba wahalifu wako ndani ya jamii hivyo kuitaka jamii kuwafichua wahalifu hao ili kukomesha vitendo vya ukatili vinavyoendelea mkoani Shinyanga.


Naye mwenyekiti wa mtaa wa Masekelo kata ya Masekelo yalikofanyika mazishi ya mtoto huyo bwana Peter Juma Kitundu alisema kifo cha mtoto huyo kinatia simanzi kubwa kwani kimesababishwa na binadamu huku akiiomba serikali kulifanyia uchunguzi wa kina tukio hilo  na lisiingizwe suala la siasa.

Kwa upande wake mwinjilisti  Emmanuel Donald Kaswalala aliyeendesha ibada ya mazishi alilaani vitendo vya kikatili wanavyofanyiwa watotot huku akiiomba jamii kumrudia mwenyezi mungu kwa kuondokana na matendo mabaya.

AUAWA NA RAIA BAADA YA KUVUNJA GETI MBEYA


 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Patrick Mgeni, umri kati ya miaka 30 – 35 aliuawa kwa kupigwa na wananchi walioamua kujichukulia sheria mkononi kwa kukatwa na vitu vyenye ncha kali sehemu za kichwani, mikononi, mgongoni na sehemu mbalimbali za mwili wake.
Tukio hilo limetokea  tarehe 27.08.2014 majira ya saa 04:30 usiku huko Nsalaga, kata ya Nsalaga, tarafa ya Iyunga, jiji na mkoa wa Mbeya. Inadaiwa kuwa, marehemu alivunja geti katika nyumba ya mama mmoja aitwaye Frola Mwaijunga (30) mkazi wa nsalaga ambapo mama huyo alishituka na kisha kupiga kelele za kuomba msaada na ndipo wananchi wa eneo hilo walijitokeza na kumkamata mtuhumiwa na kuanza kumpiga hali iliyopelekea kutokwa damu nyingi na alifariki dunia akiwa njiani kuelekea hospitali ya Rufaa Mbeya kwa matibabu.
Hakuna mtu/watu waliokamatwa kuhusiana na tukio hilo. Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa Mbeya.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Ahmed Z. Msangi anatoa wito kwa jamii kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi kwani ni kinyume cha sheria na badala yake wajenge tabia ya kuwafikisha watuhumiwa wanaowakamata kwa tuhuma mbalimbali katika mamlaka husika kwa hatua zaidi za kisheria.

Thursday, 28 August 2014

KERO KATIKATI YA JIJI LA MBEYA: MACHINGA WAJIACHIA WAPANGA BIDHAA MPAKA BARABARANI , WAHUSIKA WAMEUCHUNA, JE MAPATO HAYA YANAENDA WAPI? NA NI SAHIHI HAWA WATU KUWA HAPA?

Imekuwa ni moja ya kero kubwa na uchafuzi wa jiji katika Lango la Jiji eneo ambalo wageni , Viongozi wakubwa na watu mbalimbali wanapita.
Kero hii ambayo wahusika mnaliona hili na mnalikalia kimya linawapa watu maswali mengi sana na mpaka kudhania labda ni kamradi kamtu na ambako hakaeleweki eleweki kuwa pato lake linaenda wapi
Sio pengine ni kakipande tuu kutoka Eneo la Benki ya CRDB hadi Eneo la BP kona ya kuelekea Posta. Inafahamika kuwa eneo hili lilikatazwa kufanyika biashara lakini sasa imekuwa ndio eneo la watu kuweka Bidhaa zao na kila siku watu hawa wanazidi
Je Wahusika mpo na mnalizungumziaje?
 Hapa kila mtu anaweka Bidhaa zake wenye Nguo , Viatu na vitu mbalimbali wote wapo hapa
 Kila mmoja yupo Huru tuu
 Hapa ni nje ya wakusanya mapato(TRA) wanakazana kufukuza watu wengine maeneo mengine je hawa hawawaoni? 
 Pamegeuka Duka
 Kila kitu kinapatikana eneo hili
 Hii njia ya kuelekea Posta unakaribishwa na Viatu 
 Wengine ndio kwanza wanaanza weka mzigo
 Kila mmoja anawahi kuanza biashara
 Wale Mgambo wa Jiji ina maana hapa hawakupangiwa kupita?
 Wadau hili si ni Duka kabisa!
 Je sasa hapa hawa ni Machinga ama wafanya biashara?
Hata bei zao ukigusa hapa sio za Machinga....

MTOTO AGONGWA NA GARI NA KUFARIKI VWAWA MBEYA


Mtoto mwenye umri wa miaka 09 aliyefahamika kwa jina la Nelly Alick mkazi wa Mlolo amefariki muda dunia muda mfupi wakati anapatiwa matibabu katika hospitali ya wilaya ya Mbozi baada ya kugongwa na gari lenye namba za usajili T.257 CRP aina ya Toyota Noah lililokuwa likiendeshwa na Lameck Madihan (34) mkazi wa Mlolo.
Ajali hiyo imetokea jana majira ya saa 09:30 alasiri huko maeneo ya Karasha, kata na tarafa ya Vwawa, wilaya ya Mbozi, mkoa wa Mbeya katika barabara ya Mbeya/Tunduma. Chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi. Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya wilaya Mbozi. Dereva amekamatwa na gari lipo kituoni.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Ahmed Z. Msangi anatoa wito kwa madereva kuwa makini wanapotumia vyombo vya moto ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika. Aidha, anatoa wito kwa watembea kwa miguu kuwa makini wanapotumia barabara ili kuepuka madhara yanayoweza kuepukika.

EBOLA YAZUA BALAA NIGERIA…SHULE ZOTE ZAFUNGWA

 Madaktari wengi wameambukizwa Ebola.

Shule zote nchini Nigeria zilizokuwa zianze muhula mpya jumatatu zimeagizwa kuahirisha siku ya kufungua muhula hadi oktoba tarehe 13 kama moja wapo ya njia za kuzuia kuenea kwa viusi vya Ebola.

Waziri wa elimu aliamuru zisifunguliwe ili kuwapa walimu mafunzo jinsi ya kushughulikia ugonjwa huo.
Watu watano wamekufa kufuatia mambukizi ya homa ya ebola nchini Nigeria .
 
Takwimu za maambukizi ya Ebola
Ugonjwa huu uliozuka Magharibi mwa Afrika hasa Guinea, Liberia na Sierra Leone umewauwa zaidi ya watu 1,400 .
Huu ndio uzukaji mkubwa zaidi ambapo watu 2615 wanakadiria kuambukizwa na angalau nusu yao kuaga dunia.
Virusi hivi vinaenezwa kwa wanadamu kupitia maji maji ya mwili .
 
Takwimu za maambukizi ya Ebola
Ugonjwa huuu hauna tiba, ila kwa kuangaliwa vyema bila shaka mtu anaweza kuishi zaidi.
Ulienea Nigeria nchi iliyo na watu wengi zaidi mwezi Julai baada ya mtu aliyekuwa na virusi kutua nchini humo kutoka Liberia.
Serikali ya Nigeria inatarajia kukomesha kuenea zaidi kwa ugonjwa huu kwani sasa ni mtu mmoja tu aliye na ugonjwa huo wa ebola .
Waziri wa elimu Ibrahim Shekarau amesema Inatarajiwa angalau wafanyikazi wawili kila shule katika zile za umma na za kibinafsi watapata mafunzo maalum ya ugonjwa huu kufikia septemba 15 jinsi ya kupambana na visa vinavyoshukiwa kuwa vya Ebola
Shirika la Afya duniani WHO lilisemakuwa mlipuko huu wa ugonjwa wa Ebola imewaambukiza madaktari wengi sana.
WHO ilitoa taarifa ambayo ilionesha kuwa zaidi ya watu 2600 Guinea ,Liberia,Nigeria na Sierra Leone wameugua ugonjwa huu ulioanza mei pamoja na wafanyakazi wa huduma za afya 240.
school
Maambukizi kwa wafanyi kazi wa afya yanatokana na uhaba wa vifaa vya kujipinga na wafanyikazi kwani daktari mmoja anawahudumia wagonjwa 100,000 katika nchi zingine.
WHO ilisema kuendelea kwa madaktari kuambukizwa virusi kunapelekea juhudi za kuzuia ugonjwa huu kudidimia kwani hospitali zingine zimeanza kufungwa.
 
Ebola ilivyoenea Afrika
Ebola imewauwa madaktari wa kutajika Sierra Leone na Liberia na kupokonya nchi hizi si tu madaktari wenye uzoefu na wanaojitolea bali waliotaka kuwa mashujaa.
Mkuu wa afya wa amarekani aliyezuru nchizilizoambukizwa zaidi Liberia, Sierra Leone na Guinea alisema virusi hivyo vilionekana kutawala ingawa wataalamu walikuwa na namna ya kuukomesha.
Daktari Tom Frieden mkurugenzi wa Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Marekni alisema kuwa Ingawa virusi hivi vinaenea,Juhudi nyingi zinafanywa na kutapatikana ruzuku karibuni.