Imekuwa
ni moja ya kero kubwa na uchafuzi wa jiji katika Lango la Jiji eneo
ambalo wageni , Viongozi wakubwa na watu mbalimbali wanapita.
Kero
hii ambayo wahusika mnaliona hili na mnalikalia kimya linawapa watu
maswali mengi sana na mpaka kudhania labda ni kamradi kamtu na ambako
hakaeleweki eleweki kuwa pato lake linaenda wapi
Sio
pengine ni kakipande tuu kutoka Eneo la Benki ya CRDB hadi Eneo la BP
kona ya kuelekea Posta. Inafahamika kuwa eneo hili lilikatazwa kufanyika
biashara lakini sasa imekuwa ndio eneo la watu kuweka Bidhaa zao na
kila siku watu hawa wanazidi
Je Wahusika mpo na mnalizungumziaje?
Hapa kila mtu anaweka Bidhaa zake wenye Nguo , Viatu na vitu mbalimbali wote wapo hapa
Kila mmoja yupo Huru tuu
Hapa ni nje ya wakusanya mapato(TRA) wanakazana kufukuza watu wengine maeneo mengine je hawa hawawaoni?
Pamegeuka Duka
Kila kitu kinapatikana eneo hili
Hii njia ya kuelekea Posta unakaribishwa na Viatu
Wengine ndio kwanza wanaanza weka mzigo
Kila mmoja anawahi kuanza biashara
Wale Mgambo wa Jiji ina maana hapa hawakupangiwa kupita?
Wadau hili si ni Duka kabisa!
Je sasa hapa hawa ni Machinga ama wafanya biashara?
Hata bei zao ukigusa hapa sio za Machinga....
No comments:
Post a Comment