WASANII waliokuwa wakipigania cheo cha urais wa Manzese, Hamad Ally ‘Madee’, na Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, hatimaye wamemaliza tofauti zao baada ya kudumu kwenye bifu kwa muda mrefu.
Mkali wa Bongo fleva,Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’.
Ishu hiyo imejidhihirisha
kwenye mbio za Serengeti Fiesta 2013, ambapo muda mwingi wamekuwa
wakishirikiana kwenye kazi zao za muziki na hata kupeana lifti na
kupanda gari moja jambo ambalo hapo mwanzo lilikuwa haliwezekani.
Rais wa Manzese, Hamad Ally ‘Madee’.
Agosti 23, mwaka huu wasanii hao walitinga jijini Tanga pamoja wakitokea Dar ambapo Nay wa Mitego ndiye aliyekuwa amepewa lifti kwenye gari ya Madee, bila hiyana Nay alisisitiza kwamba wamemalizana kimyakimya.
“Yale yalikuwa mambo ya jukwaani zaidi, tumeyamaliza, kwa sasa tuko poa,” alisema Nay.
No comments:
Post a Comment