STAILI
ile ile waliyotumia Yanga SC kumpata mshambuliaji Emmanuel Arnold Okwi
ndiyo ambayo klabu yake ya zamani, Simba SC inaitumia kumrejesha kundini
Mganda huyo.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari jioni hii mjini Dar es Salaam, Okwi amesema
kwamba amesaini Simba SC mkataba huru wa muda, baada ya Yanga SC kumpa
barua ya kusitisha mkataba naye jana pamoja na kumshitaki Shirikisho la
Soka Tanzania (TFF).
Okwi
amesema ameamua kuomba kuichezea Simba SC kipindi hiki ambacho ana
matatizo na Yanga SC ili kulinda kipaji chake, kwa kuwa hata FIFA
haitaki mchezaji akae bila kucheza.
“Sasa wakati Yanga wanaendelea na kesi yao, mimi ninaomba nichezee Simba SC ili kulinda kipaji changu. Nimewaandikia barua TFF na FIFA pia na nina matumaini usajili wangu utaidhinishwa, kwa sababu mimi si tatizo katika hili,”amesema. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema kwamba wamemsaini mchezaji huyo baada ya kupitia kwa kina suala lake na Yanga SC na kugundua haki ipo upande wa mchezaji. “Baada ya kulipitia suala lake na Yanga kwa undani kabisa na vielelezo ambavyo mchezaji mwenyewe ametupatia, tumejiridhisha tuko sahihi kumsaini ili acheze mpira kunusuru kipaji chake kipindi hiki ambacho ana matatizo na Yanga SC,”amesema Poppe.
Tayari
Simba SC imetuma jina la mchezaji huyo katika usajili wake TFF na
ataungana na Mganda mwenzake, Joseph Owino, Warundi Pierre Kwizera na
Amisi Tambwe na Mkenya, Paul Kiongera katika wachezaji watano wa kigeni.
“Tumewaandikia
barua TFF kuomba kumtumia mchezaji huyu kwa muda wakati kesi yake na
Yanga inaendelea, tumeambatanisha na barua yake ambayo yeye anatuomba
kucheza kwetu kulinda kipaji chake,”amesema Poppe.
Okwi
aliichezea Simba SC tangu mwaka 2009 kabla ya Januari mwaka jana kuuzwa
kwa dola za Kimarekani 300,000 Etoile du Sahel ya Tunisia.
Etoile
haikulipa fedha hizo Simba SC na baadaye ikaingia kwenye mgogoro na
Okwi, aliyedai hakulipwa pia mishahara yake kwa miezi mitatu.
Okwi
akawafungulia Etoile kesi FIFA na akaomba wakati mgogoro wao
unaendelea, aruhusiwe kuchezea timu yoyote kulinda kipaji chake, ndipo
akajiunga na SC Villa ya kwao.
Akiwa
SC Villa ndipo aliposaini Yanga SC Desemba mwaka jana na pamoja na
mapingamizi yaliyoanzia ndani, na baadaye klabu yake, Etoile- lakini
Okwi aliidhinishwa kuichezea timu hiyo ya Jangwani.
Okwi
aliichezea Yanga SC mechi 11 na kuifungia mabao matano- lakini kuelekea
mechi tano za mwisho za Ligi Kuu msimu uliopita akaingia kwenye mgogoro
na klabu hiyo.
Okwi
alisusa kushinikiza amaliziwe fedha zake za usajili na mgogoro wao
umeendelea huku mchezaji huyo akiwa amesusa tangu Machi, miezi minne tu
baadaye tangu asajiliwe.
Vikao
kadhaa vimekwishafanyika baina ya Okwi na Yanga SC tangu hapo kutafuta
suluhu ya suala hilo na kikao cha mwisho leo baina ya mchezo huyo na
Mwenyekiti wa klabu hiyo, Yussuf Manji matokeo yake ni nyota huyo
kurejea Msimbazi.
Kuhusu
deni lao la dola 300,000 kumuuza mchezaji huyo Etoile, Poppe amesema
haihusiani kabisa na usajili wake huu wa sasa. “Ile kesi yetu ya madai
ya fedha zetu kule FIFA ilikwishamalizika na vielelezo vyote
vilipelekwa, bado kutolewa hukumu tu,” amesema.
“Sasa wakati Yanga wanaendelea na kesi yao, mimi ninaomba nichezee Simba SC ili kulinda kipaji changu. Nimewaandikia barua TFF na FIFA pia na nina matumaini usajili wangu utaidhinishwa, kwa sababu mimi si tatizo katika hili,”amesema. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amesema kwamba wamemsaini mchezaji huyo baada ya kupitia kwa kina suala lake na Yanga SC na kugundua haki ipo upande wa mchezaji. “Baada ya kulipitia suala lake na Yanga kwa undani kabisa na vielelezo ambavyo mchezaji mwenyewe ametupatia, tumejiridhisha tuko sahihi kumsaini ili acheze mpira kunusuru kipaji chake kipindi hiki ambacho ana matatizo na Yanga SC,”amesema Poppe.
Yanga mtanikoma; Okwi akiwa ameshika jezi yake nbamba 25 kwa pamoja na Hans Poppe |
No comments:
Post a Comment