Mcheza shoo wa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond,’ Moses Iyobo
amefunguka kwa mara ya kwanza baada ya kuenea uvumi wa kutoka kimapenzi
na mcheza filamu mahiri Bongo, Aunt Ezekiel kuwa hawezi kumuacha msanii
huyo ng’o.
Akizungumza hivi karibuni, Moses alisema kuwa kutokana na
maneno mengi kuenea kuwa anatoka na Aunt, ameona ni bora aweke wazi
hisia zake kwamba ni kweli anampenda msanii huyo na kuwa naye mbali
itakuwa vigumu.
“Mengi yameongelewa sana sasa naweka wazi kuwa nampenda sana Aunt.
Unajua kama mtu haukuwa na uhusiano naye mara unaanza kusikia vitu vya
ajabu bora tu ufanye kweli hata kama wanakusema wakuseme kihalali na si
vitu ambavyo si vya kweli,” alisema dansa huyo ambaye ni mume wa
mwanamke aliyefahamika kwa jina moja la Mwegi.
No comments:
Post a Comment