Friday, 29 August 2014

TFF YAIBEBA YANGA


jaja

Shirikisho la soka nchini, TFF limesogeza mbele muda wa usajili kwa klabu za ligi kuu na ligi daraja la kwanza kwa masaa 48 zaidi, Siku mbili kwa wachezaji wa ndani na wiki moja zaidi kwa usajili wa wachezaji wa kigeni kutoka nje ya nchini. Uamuzi huo umefikiwa baada ya klabu zote 14 za ligi kuu na 15 za ligi daraja la kwanza kushindwa kukamilisha taratibu za uhamisho wa Kieloktroniki. Ni timu moja tu iliyoweza kukamilisha usaajili wake siku ya jana ambayo ilikuwa ni ya mwisho baada ya mara mbili kuongezwa kwa muda.
Yanga SC wameshindwa kupata hati ya uhamisho wa kimataifa ( ITC) ya mshambulizi, Geilson Santos ‘ Jaja’ na kuna uwezekano mkubwa wa mchezaji huyo kutoka Brazil akaondolewa kat
ika timu hiyo. Katikati ya mwaka 2010 timu hiyo ilishindwa kukamilisha taratibu za kumuhamisha mshambulizi raia wa Ghana, Keneth Asamoah aliyekuwa akichezea klabu ya FK Jagodina ya Serbia.
Jaja anaweza kutemwa na kuwapisha Waganda, Hamis Kizza na Emmanuel Okwi kuungana na wachezaji wengine wa kimataifa, Haruna Niyonzima, Mbuyu Twite na Andry Coutinho. Jina la mchezaji halipo katika orodha ya wachezaji wa Yanga na hakuna maombi yoyote ambayo uongozi wa Yanga umewasilisha kwa shirikisho la soka nchini, TFF hadi kufikia siku ya jana. Kama mshambulizi huyo atakwama kusajiliwa kama ilivyokuwa kwa Asamoah huku akiwa na mkataba wa miaka miwili uongozi hautakwepa lawama hivyo wanatakiwa kufanya kila wawezalo na si kujiaminisha kupata msaada wa muda mrefu kutoka kwa Okwi, na Kizza.
Afadhali kwa Kizza yeye ni mchezaji wa Yanga hasa ila Okwi ataendelea kuwasumbua Yanga.
Uongozi wa Yanga unasema kuwa kumekuwa na tatizo la mawasiliano kati yao na Shirikisho la soka la Brazil, CBF, ila hawajafanya jitihada za kupeleka maombi hayo rasmi kwa TFF ambao watafanya mawasiliano na wenzao wa Brazil ili kuhakikisha mchezaji huyo anasajiliwa na kukamilisha taratibu zote.
Itakuwa ni sawa na kukosa umakini kwa viongozi wa Yanga kwa kuwa wamekuwa wakifahamu, Jaja ni mchezaji wao mpya tangu mwezi uliopita. Mfumo wa TMS umekuwa ukiwasumbua viongozi wa klabu za Tanzania lakini maombi ya uhamisho wa wachezaji yanayofanywa kutumia mfumo huo hufanyika haraka.

SaSA Yanga wamepata muda zaidi wa kufikiria kwa umakini ni mchezaji gani wa kigeni anayetakiwa kuachwa kati ya washambuliaji hao watatu. Kulikuwa na uwezekano mkubwa wa Jaja kuachwa, lakini matumaini ya Mbrazil huyo kucheza Tanzania yamerejea baada ya muda zaidi wa usajili kuongezwa.

No comments:

Post a Comment