Friday, 29 August 2014

AUAWA NA RAIA BAADA YA KUVUNJA GETI MBEYA


 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Patrick Mgeni, umri kati ya miaka 30 – 35 aliuawa kwa kupigwa na wananchi walioamua kujichukulia sheria mkononi kwa kukatwa na vitu vyenye ncha kali sehemu za kichwani, mikononi, mgongoni na sehemu mbalimbali za mwili wake.
Tukio hilo limetokea  tarehe 27.08.2014 majira ya saa 04:30 usiku huko Nsalaga, kata ya Nsalaga, tarafa ya Iyunga, jiji na mkoa wa Mbeya. Inadaiwa kuwa, marehemu alivunja geti katika nyumba ya mama mmoja aitwaye Frola Mwaijunga (30) mkazi wa nsalaga ambapo mama huyo alishituka na kisha kupiga kelele za kuomba msaada na ndipo wananchi wa eneo hilo walijitokeza na kumkamata mtuhumiwa na kuanza kumpiga hali iliyopelekea kutokwa damu nyingi na alifariki dunia akiwa njiani kuelekea hospitali ya Rufaa Mbeya kwa matibabu.
Hakuna mtu/watu waliokamatwa kuhusiana na tukio hilo. Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa Mbeya.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Ahmed Z. Msangi anatoa wito kwa jamii kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi kwani ni kinyume cha sheria na badala yake wajenge tabia ya kuwafikisha watuhumiwa wanaowakamata kwa tuhuma mbalimbali katika mamlaka husika kwa hatua zaidi za kisheria.

No comments:

Post a Comment