Msanii wa filamu, Salma Omary ‘Sabby’ ameamua kufunguka kuwa ameteswa
sana na rushwa ya ngono aliyokuwa akikutana nayo pindi alipokuwa
akifurukuta kutoka kisanii.
Akizungumza Sabby alisema, tatizo hilo la rushwa anaweza
kuwa miongoni mwa wasanii waliosumbuliwa sana wakati kuna baadhi
walipokuwa wakitolewa nje, walikuwa wanajenga bifu naye na wengine
kumtishia kumharibia.
“Mimi kitu ambacho kinaniumiza sana mpaka leo ni jinsi wanawake
tunavyodhalilishwa kila siku, naumia mno nimepita katika tabu nyingi
mpaka nafikia hapa leo, ila namshukuru Mungu siku zote,” alisema Sabby
ambaye ameng’ara kwenye filamu kama vile Siri ya Gining, Hard Price,
Moto wa Radi, Dr. Ray na nyinginezo.
No comments:
Post a Comment