Shule zote nchini Nigeria zilizokuwa zianze muhula mpya jumatatu zimeagizwa kuahirisha siku ya kufungua muhula hadi oktoba tarehe 13 kama moja wapo ya njia za kuzuia kuenea kwa viusi vya Ebola.
Waziri wa elimu aliamuru zisifunguliwe ili kuwapa walimu mafunzo jinsi ya kushughulikia ugonjwa huo.
Watu watano wamekufa kufuatia mambukizi ya homa ya ebola nchini Nigeria .
Ugonjwa huu uliozuka Magharibi mwa Afrika hasa Guinea, Liberia na Sierra Leone umewauwa zaidi ya watu 1,400 .
Huu ndio uzukaji mkubwa zaidi ambapo watu 2615 wanakadiria kuambukizwa na angalau nusu yao kuaga dunia.
Virusi hivi vinaenezwa kwa wanadamu kupitia maji maji ya mwili .
Ugonjwa huuu hauna tiba, ila kwa kuangaliwa vyema bila shaka mtu anaweza kuishi zaidi.
Ulienea Nigeria nchi iliyo na watu wengi zaidi mwezi Julai baada ya mtu aliyekuwa na virusi kutua nchini humo kutoka Liberia.
Serikali ya Nigeria inatarajia kukomesha kuenea zaidi kwa ugonjwa huu kwani sasa ni mtu mmoja tu aliye na ugonjwa huo wa ebola .
Waziri
wa elimu Ibrahim Shekarau amesema Inatarajiwa angalau wafanyikazi
wawili kila shule katika zile za umma na za kibinafsi watapata mafunzo
maalum ya ugonjwa huu kufikia septemba 15 jinsi ya kupambana na visa
vinavyoshukiwa kuwa vya Ebola
Shirika la Afya duniani WHO lilisemakuwa mlipuko huu wa ugonjwa wa Ebola imewaambukiza madaktari wengi sana.
WHO
ilitoa taarifa ambayo ilionesha kuwa zaidi ya watu 2600 Guinea
,Liberia,Nigeria na Sierra Leone wameugua ugonjwa huu ulioanza mei
pamoja na wafanyakazi wa huduma za afya 240.
Maambukizi
kwa wafanyi kazi wa afya yanatokana na uhaba wa vifaa vya kujipinga na
wafanyikazi kwani daktari mmoja anawahudumia wagonjwa 100,000 katika
nchi zingine.
WHO
ilisema kuendelea kwa madaktari kuambukizwa virusi kunapelekea juhudi
za kuzuia ugonjwa huu kudidimia kwani hospitali zingine zimeanza
kufungwa.
Ebola
imewauwa madaktari wa kutajika Sierra Leone na Liberia na kupokonya
nchi hizi si tu madaktari wenye uzoefu na wanaojitolea bali waliotaka
kuwa mashujaa.
Mkuu
wa afya wa amarekani aliyezuru nchizilizoambukizwa zaidi Liberia,
Sierra Leone na Guinea alisema virusi hivyo vilionekana kutawala ingawa
wataalamu walikuwa na namna ya kuukomesha.
Daktari
Tom Frieden mkurugenzi wa Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa
Marekni alisema kuwa Ingawa virusi hivi vinaenea,Juhudi nyingi
zinafanywa na kutapatikana ruzuku karibuni.
No comments:
Post a Comment