MAPENZI bwana! Baada ya
kuogelea kwa muda mrefu katika penzi la muigizaji Kajala Masanja,
hatimaye shemeji wa aliyekuwa rafiki wa mwigizaji huyo, Wema Sepetu,
Ahmed Hashimu ‘Petit Man’ ametangaza ndoa na dada wa Mbongo Fleva,
Nasibu Abdul ‘Diamond’, Esma Abdul.
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini kilicho karibu na Diamond na Wema
ambao penzi lao lilipata ‘mushkeli’ kidogo hivi karibuni, Petit Man
tayari ameshakamilisha kila kitu kinachotakiwa kufanyika kabla ya ndoa
na kilichobaki ni kutamka siku husika tu.
Kilidai kuwa, Petit alichukua uamuzi huo
baada ya kushauriwa na Wema kuwa umri unakwenda na vishawishi ni vingi
hivyo ni bora aoe mapema.“Unajua Petit Man anamheshimu sana Wema kwa
hiyo alipomwambia Petit kuwa umri unazidi kwenda na anahitaji kuwa na
familia yake akaukubali ushauri wake,” kilinyetisha chanzo hicho.
Baada ya kupata maelezo hayo, MPANDA FM lilimtafuta Petit Man na
kumuuliza kuhusiana na ishu hiyo, bila kuumauma maneno alikiri.“Ni kweli
mama (Wema) aliniweka chini na kuniambia kuwa umri unakwenda hivyo
nahitaji niwe na familia yangu kwa hiyo siwezi kuwa na familia bila ya
kuwa na mke ndipo aliponichagulia mke ambaye ni dada yake wa damu kabisa
na Nasibu Abdul ‘Diamond’ anayeitwa Esma na kwa taarifa yako tu, tayari
nimeshakamilisha kila kitu,” alisema Petit.
Alipoulizwa kuhusiana na wanawake aliowahi kuwa nao kipindi cha nyuma
akiwemo Kajala, Petit alisema huko kote ilikuwa ni njia ya kuelekea
kwenye kilele cha mafanikio ambayo ni ndoa yake na Esma.
“Acha nipumzike na madhira ya dunia maana huko kote nilipopita
hakukuwa chaguo langu ila kwa Esma nimekufa nimeoza bado kuzikwa tu
yaani mimi ni mfu ninayetembea mbele ya Esma.”
No comments:
Post a Comment