YP alikuwa akimpa njia Chege wakati wanarekodi wimbo wa pamoja na Tiptop Connection katika Studio za Enrico |
Saidi Juma maarufu kwa jina la Chege Chigunda Mtoto wa Mama Saidi kutoka
TMK ameumizwa sana na Msiba wa mwenzake Yessay Ambilikile Y.P na
Kuyasema haya...
"Innalilahi wa inna ilaih rajiun,sikuwahi kufikiria itatokea siku usiwe
karibu yangu nilipigania sana uwepo wako katika kundi letu,wewe ndio
ilikua remot yangu ktk uimbaji machozi yananitoka kila dakika nakumbuka
mengi naujua msaada wako kwangu,tulipendwa sana kwa sauti zetu kufanana
my brother,mungu ndio anajua kwanini ulipojitoa kundini nilipigania mpk
uongozi
ukakurudisha,umeniacha ktk Hali ngumu sana na kuiacha Tmk wanaume family
ktk majonzi makubwa yasio weza kufutika kirahisi hatuna la kufanya tena
kwa sasa tunachofanya nikubaki tunakuombea kwa mwenyezi mungu
akupunguzie adhabu na kukuweka mahala pema peponi RIP YP----pumzika
salama my brother"
No comments:
Post a Comment