Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu, Dar es Salaam imemzuia msanii kutoka Nigeria, Adedeji Adelek maarufu kama ‘Davido’ kuperform katika tamasha la Fiesta linaloandaliwa na Clouds Fm na Prime Promotion, October 18,2014.
Amri hiyo imetolewa jana (October 17) na hakimu mkazi wa mahakama ya
kisutu , mheshimiwa D. Kisoka kufuatia maombi ya dharura
yaliyowasilishwa mahakamani hapo na Times Fm Radio na Times Fm
Promotion.
Times Fm Radio na Times Fm Promotion walipeleka maombi ya dharura
mahakamani hapo wakiitaka mahakama kumzuia msanii huyo kuperform katika
tamasha hilo kwa kuwa licha ya BASATA (Baraza La Sanaa Tanzania) kukataa
kutoa kibali cha msanii huyo kwa maelezo kuwa tayari alikuwa
ameshachukuliwa kibali cha kuperform nchini November 1 kwenye tamasha
lililoandaliwa na Times Fm Radio, Clouds Fm na Prime Times Promotion
waliendelea na taratibu zote bila kujali zuio hilo la BASATA.
Times Fm Radio na Times Fm Promotion waliiomba mahakama kuidhinisha
madai yao dhidi ya Clouds Fm, Prime Promotion na mkurugenzi wa kampuni
inayomsimamia Davido, HKN Music.
Madai hayo ni pamoja na kulipwa fidia ya gharama na usumbufu
waliosababishiwa na walalamikiwa kadiri Mahakama itakavyoona inafaa.
Mahakama imetoa amri kuwa msanii huyo amezuiwa kufanya onesho hilo
October 18,2014 hadi pale ufumbuzi wa kesi hiyo utakapopatikana
mahakamani hapo.
Awali, Davido alisikika katika matangazo ya Times Fm Radio akieleza
kuwa atakuja Tanzania November 1 kwa ajili ya kufanya onesho
linaloandaliwa na kituo hicho cha radio lililopewa jina la ‘The Climax’.
No comments:
Post a Comment