Monday, 20 October 2014

Picha: Gerard Pique Awatolea Uvivu Askari Wa Usalama Barabarani



Beki kutoka nchini Hispania na klabu ya Barcelona, Gerard Piqué i Bernabeu, ameshindwa kujizuia na kujikuta akiwabwatukia askari wa usalama barabarani, kufuatia adhabu ya kulipishwa faini iliyomuangukia.
Pique, alikumbana na kadhia hiyo wakati akirejea nyumbani baada ya kuitumikia timu yake ya taifa ambayo inaendelea na mchakato wa kusaka nafasi ya kutetea ubingwa wa barani Ulaya mwaka 2016.
Hata hivyo chanzo cha habari hizi kimeeleza kwamba kosa lililopelekea beki huyo wa kati wa Barcelona kulambwa faini, lilisababishwa na nduguye baada ya ya kuegesha vibaya gali walilokuwa wamepanda katika kituo cha mabasi, na kujikuta wakisababisha foleni kwa muda wa dakika 15.
Kutokana na hali hiyo Pique, alionesha hasira na kuanza kuwatolea maneno makali askari waliofuatilia makosa yaliyokuwa yanawakabili, ambapo aliwambia huenda wanashobokea faini kutokana na umaarufu alionao.
Aliwaambia askari hao kwamba walifanya hivyo kwa lengo la kujipatia fedha kirahisi kwa kutambua katu hawezi kuwagomea kufanya hivyo kutokana na hali halisi inayomkabili (Uamaarufu).
Lakini pamoja na purukushani hizo zilizochukua muda mfupi, Pique alijua amefanya makosa na mwishowe aliwataka radhi askari hao, na kisha aliendelea na safari ya kurejea nyumbani kwake.

No comments:

Post a Comment