Kitendo hicho kiliwaacha wananchi vinywa wazi wasijue la kufanya huku
wakibaki kupiga picha kwa kutumia simu zao za mikononi.Mapema wiki hii
katika kijiji cha Oshindi nchini Nigeria wananchi walishuhudia sinema ya
bure ambapo kamera zao zilikuwa macho yao na simu zao pale ndege
aliyekuwa anapaa angani ghafla alianguka chini baada ya kudandia nyaya
za umeme na kugeuka mwanamke.
Mwanamke huyo alionekana kuchubuka na kuwa na vidonda katika mwili wake hali iliyo kuwa inahuzunisha huku akiwa haongei (bubu).
Wananchi hao walimuuliza maswali mengi wakitaka kujua imekuaje hadi akageuka binadamu wakati yeye alikuwa ndege anapaa juu.
Mama huyo aliwajibu kuwa alikuwa anaenda kumtazama binti yake aliyekuwa amejifungua muda mchache.
Habari zinasema kuwa mwanamke huyo alikuwa mchawi na binti yake
alikuwa anafanya sala wakati yule mama alikuwa anapaa. Inaelezwa kuwa
wakati sala inaendelea ndipo mwanamama huyo aliyekuwa amejibadilisha na
kuwa ndege akageuka binadamu.
Taarifa zinaarifu kuwa binti yake alikuwa kila akijifungua mtoto anafariki papo hapo.
No comments:
Post a Comment