Shirika
la afya duniani, WHO limearifu kuwa liko mbioni kufanya majaribio ya
chanjo dhidi ya ugonjwa wa Ebola, ambao umeripotiwa kuua takribani watu
4,500 huku nchi za Afrika Magharibi zikiripotiwa kuathirika zaidi tangu
kulipuka kwa ugonjwa huo.
Taarifa iliyoripotiwa na CNN imesema
kuwa shirika hilo limepanga kuanza utekelezaji wa jaribio hilo mapema
Januari mwaka 2015 katika nchi za Afrika Magharibi, huku wakisisitiza
kuwa chanjo zote hazina madhara kwa afya ya binadamu, japo chanjo hiyo
haitowahusu wagonjwa ambao tayari wana maambukizi Ebola.
Mratibu
wa zoezi hilo Dk. Marie Paule Kieny amesema, chanjo hiyo itatolewa kwa
mtu yoyote atakayekuwa tayari kujitolea kushiriki.
Amezitaja nchi za Mali, Uingereza na Marekani kuwa ni baadhi ya nchi ambazo jaribio la chanjo hiyo litafanyika.
Shirika
la afya limesema limeagiza wataalamu kufanya ziara Afrika Magharibi
katika nchi ambazo wananchi wake wameathirika zaidi na ugonjwa huo,
ambapo pia ziara hiyo itahusisha pia zoezi la ukaguzi wa vituo ambavyo
vitatumika kutolea huduma hiyo ya chanjo.
Iwapo
chanjo hii itafanikiwa itafufua matumaini kwa watu wa Afrika ya
Magharibi ambao wameshuhudia athari kubwa zilizosababishwa na Ebola
ambapo watu zaidi ya 4,500 wameripotiwa kufariki na wengine zaidi ya
9,000 wana maambukizi ya ugonjwa huo
No comments:
Post a Comment