Mchezaji tennis kutoka nchini Uingereza Andy Murray amefanikiwa kumshinda David Ferrer katika michuano ya wazi ya Vienna inayofanyika nchini Austria kwa muda wa majuma amwili.
Murray amemshinda mpinzani wake kutoka nchini Hispania kwa idadi ya seti mbili kwa moja ambazo ni 5-7 6-2 na 7-5.
Kwa ushindi huo Andy Murray anapiga hatua na kutinga kwenye mtanange wa fainali.
Hii inakuwa ni mara ya tatu kwa Murray mwenye umri wa miaka 27, kumshinda Ferrer, katika hatua ya nusu fainali.
Muda mfupi baada ya mchezo huyo kumalizika huko mjini Vienna, Murray aliwaambia wandishi wa habari hana budi kushukuru baada ya kumaliza wiki katika hali ya furaha, ambayo imesababishwa na ushindi uliopatikana katika mchezo uliochukua saa mbili na dakika 42.
Ameongeza kuwa mchezo huo ulikuwa mgumu kwake ukizingatia umuhimu wake katika kufuzu kuelekea fainali za London.
No comments:
Post a Comment