Tuesday 1 April 2014

Diamond Kwenye Tuzo Kubwa Africa,Kilio Chake Kikubwa Kwako Kiko Hapa!

Msanii Diamond Platnumz, ameendelea kuchana mawimbi katika anga la muziki hususan kwa upande wa Afrika ambapo amefanikiwa kuingia katika orodha ya wasanii 20 Bora ambao wanafanya vizuri Afrika, ambao wataingia katika kinyanganyiro cha kuwania tuzo za Kora.

Diamond katika orodha hii, anatokea sambamba na majina ya wasanii wakubwa Afrika, kama vile Oliver Mtukudzi, Fally Ipupa, Mafikizolo pamoja na wakali wengine wa muziki barani Afrika.
Kutokea kwa Diamond katika orodha hii, ni nafasi nyingine kubwa ya kuipeperusha bendera ya Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla, katika jukwaa la kimataifa.
Kwa sasa mchakato unaendelea kupitia ukurasa wa facebook wa Tuzo hizi, ambapo maoni mbalimbali ya mashabiki yanakushanywa kuhusiana na wasanii gani wanaokubalika zaidi, tayari kwa kuwapambaniza katika tuzo hizo kubwa.
dd 2dd

No comments:

Post a Comment