BEHRAMPUR , India
Dhoruba kubwa imeikumba nchi ya India kufuatia
mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali (kimbunga) kunyesha kwenye ukanda wa pwani ya mashariki ya India jumamosi
jioni na kuleta uharibifu mkubwa wa makazi ya watu huku maelfu wakiyahama
makazi yao na kutafuta hifadhi salama
![]() |
wimbi kubwa likielekea pwani kwenye bandari ya Jalaripeta kwenye wilaya ya Visakhapatnam kusini mwa nchi ya India na kuharibu makazi zaidi ya 10,000 |
Barabara zote zilikukuwa tupu wakati mawimbi
makubwa yalipoingia kwenye mwambao wa mji wa Orissa , ambao ulikumbwa na Kimbunga
kikali. Jumamosi mchana.
![]() |
wanakijiji walioathiriwa na kimbunga, wakipata chakula katika hifadhi ya muda huko Chatrapur kilometa 200 |
Upepo mkali uliotishia hata wanaume watu wazima
ulivuma kwenye mji huo. Maji ya bahari yalisukumwa kuelekea nchi kavu na
kukumba vijiji vilivyokaliwa na wakulima wadogowadogo vyenye vibanda vya matope
na nyasi.
![]() |
wake wa wavuvi wa india wakiwaashiria waume zao (wavuvi) kurudi kufuatia dalili za kimbuka |
![]() |
mwamvuli haukufaa kwa upepo mkali |
Ikiwa na eneo kubwa lenye maji ya moto
duniani, Bahari ya Hindi inachukuliwa kama chanzo cha dhoruba na baadhi ya
dhoruba zilizoleta maafa makubwa kwenye siku za karibuni ilitokea kwenye pwani
ya Bengal, ikiwa ni pamoja na kimbunga cha mwaka 1999 ambacho pia kiliikumba Orissa
na kuua watu 10,000.
![]() |
familia ikibebelea mizigo yao na kuelekea sehemu salama |
Viongozi wa serikali wanasema idadi
kamili ya vifo haijajulikana na itawekwa wazi siku ya jumapili.
Katika mji wa Behrampur , kilometa 10 (
maili 7 ) toka eneo la bara ambapo dhoruba ndio ilikuwa imelenga, anga
liliingia giza ghafla wakati dhoruba hilo lilipotua likiwa na upepo mkali
iliyoambatana na mvua nzito na kuacha mitaa yote ya mji huo ikiwa mitupu .
![]() |
waathiriki wa dhoruba hiyo wakipata chakula kwenye hifadhi ya muda |
Madirisha ya nyumba yalipasuka kutokana na upepo mkali. Huku vitu vya zilivyokuwa nje ya nyumba vikisikika kugonga kuta za nyumba.
"Wazazi wangu wamekuwa wakinipigia simu mara kwa mara ... walikuwa na wasiwasi sana ," alisema HEMANT PATI , 27, ambaye alikuwa kujificha katika hoteli na watu wengine 15 kutoka mji wa pwani ambao ulikuwa wa kwanza kukumbwa na dhoruba.
![]() |
wanakijiji walijilinda na mvua kubwa kwa kujifunika na manailoni |
Meneja wa hoteli hiyo alisema alifunga
milango dhidi ya mtu yeyote kujaribu kuingia , akisema kulikuwa na chakula,
maji na umeme wa jenereta tu kwa ajili ya wageni ya Jyoti Hoteli. "Hakuna
mtu anaweza kuja ndani , na hakuna mtu anaweza kwenda nje," Shaik
Nisaruddin alisema.
![]() |
wanaume wakijarinu kuutoa mti ulioanguka barabarani kufuatia mvua na upepo mkali octoba 12 |
Makadirio ya nguvu ya dhoruba imeshuka kidogo,kulinganisha na taarifa ya onyo
iliyotolewa na Jeshi la Maji la Marekani pamoja na kituo cha tahadhari (Typhoon
Warning Centre) jijini Hawaii iliyoonyesha uwepo upepo endelevu wenye kasi ya
kilomita 222 kwa saa ( 138 maili kwa saa ), na kupanda hadi 268 km/h (167 mph).
![]() |
wanakijiji wa india wakipambana na upepo mkali |
Ingawa dhoruba, iliendelea kuwa na nguvu
nyingi mno na hatari. Saa chache kabla ya kugonga ardhi , kiini cha dhoruba
hiyo kilitawanyika na kueneza upepo mkali kwenye maeneo mengi zaidi na
kusababisha madhara makubwa ," alisema Jeff Masters, mkurugenzi wa hali ya
hewa katika kituo binafsi cha hali ya hewa kilicho chini ya Marekani
![]() |
msichana akichungulia dirishani akiwa anasafiri kwa basi kuelekea eneo salama |
" Ni kitu kibaya pale kilipotua kwenye nchi kavu, nyumba nyingi nchini India
haziwezi kuhimili hata dhoruba dhaifu " Masters alisema.
Pia alisema si pwani pekee itapata uharibifu
mkubwa. "Hii ni dhoruba yenye nguvu na yakushangaza, itabeba upepo wa
kimbunga kuupeleka bara kwa muda wa takribani masaa 12, ambayo si kawaida
kabisa , " alisema Masters kabla ya
kutokea kwa dhoruba hiyo.
Vimbunga kawaida kupoteza nguvu vinapopiga
nchi kavu, ambapo kuna unyevu wenye joto dogo ambao huuathiri nishati nguvu ya
dhoruba.
Ijumaa jioni, baadhi ya watu zaidi ya 420,000
walihama makazi yao kuelekea kwenye hifadhi na ardhi ya juu katika mji wa Orissa,
na 100,000 zaidi katika mji jirani wa Andhra Pradesh , alisema Anil Goswami
katibu wa mambo ya ndani ya Indaia.
L.S. Rathore , mkuu wa Idara ya Hali ya
Hewa ya Hindi , alitabiri kuongezeka dhoruba kwa kipimo cha mita 3-3.5 (
10-11.5 futi) , lakini watalaam kadhaa wa Marekani walitabiri dhoruba kubwa sana ya
maji na kuelekea pwani . Ryan Maue mtaalatam wa hali ya hewa toka shirika
binafsi la Marekani (Weather Bell) alisema kuwa, hata katika mazingira
bora, ubashiri ulionesha kutakuwa na
mawimbi ya mita 7-9 (20-30 futi).
Kuongezeka kwa dhoruba ni muuaji makubwa
katika dhoruba kama ile, ingawa mvua kubwa ilichangia kuzidisha uharibifu.
Serikali ya India imeisema watu milioni 12 wataathiriwa na dhoruba, ikiwa ni
pamoja na mamilioni wanaoishi mbali na pwani.
Kulikuwa na taarifa chache za dhoruba
huko Orissa muda mchache baada ya
dhoruba kuanza kupiga, kwa Phailin tayari kulikuwa na dhoruba kubwa kwa karibu
masaa 36, na upepo mkubwa kuongezeka, alisema Maue. "Dhoruba hii kubwa haiwezi
kumalizima haraka, " alisema.
Kimbunga cha mwaka 1999 kilikuwa na nguvu
kama hiki cha Phailin lakini kilifunika eneo ndogo - kilirusha nje kama mita
5.9 (19.4 -futi).
Masaa kadhaa kabla ya dhoruba hii ,
wanakijiji wapatao 200 walikusanyika kwenye vyumba viwili, kwenye nyumba imara
ya seruji shuleni katika kijiji cha Subalaya , umbali wa kilomita 30 ( maili 20
) kutoka pwani , wakati maafisa wa mambo ya dharura ya ndani wakisambaza
chakula na maji. Barabara zote zilikuwa karibu tupu, ila kwa ajili ya malori
mawili kuleta misaada zaidi kwenye shule hiyo. Watoto walionekana kutetemeka na
kutereza katika mvua wakiwa wanashushwa kutoka kwenye malori, wakiwafuata
wanawake waliokuwa wamebeba mizigo
Wengi wenye makazi ya chini walikimbilia
kwenye hifadhi , lakini baadhi yao walibaki na jamaa zao wakihofia dhoruba
inaweza kuwakumba wakiwa njiani.
"Mtoto wangu alibaki na mke wake kwa sababu ya ng’ombe na mali ," alisema Kaushalya Jena mzee wa miaka 70 akilia kwa hofu ndani ya makazi ya muda. "Mimi sijui kama wao ni salama. "
"Mtoto wangu alibaki na mke wake kwa sababu ya ng’ombe na mali ," alisema Kaushalya Jena mzee wa miaka 70 akilia kwa hofu ndani ya makazi ya muda. "Mimi sijui kama wao ni salama. "
Huko Bhubaneshwar na katikati ya mji wa
Orissa, maafisa wa serikali na kujitolea kwa pamoja waliweka maelfu ya mifuko ya chakula kwa
ajili ya makambi ya misaada.
"Inaonekana ajabu, kwa sababu siku ilikuwa ni nzuri na jua lilikuwepo ," alisema Doris Lang wa Honolulu , ambaye alikuwa na rafiki katika mahekalu kando ya bahari kwenye mji wa Puri wakati habari za kimbunga zilipowafikia wao.
"Inaonekana ajabu, kwa sababu siku ilikuwa ni nzuri na jua lilikuwepo ," alisema Doris Lang wa Honolulu , ambaye alikuwa na rafiki katika mahekalu kando ya bahari kwenye mji wa Puri wakati habari za kimbunga zilipowafikia wao.
Kiongozi wa juu wa serikali, Waziri Kiongozi Naveen
Patnaik , amewaasa watu kuwa watulivu .
" Naomba kila mtu asiwe na hofu, Tafadhali isaidieni serikali . . Kila mtu kuanzia kijiji hadi makao makuu wanatakiwa kuwa na tahadhari," aliwaambia waandishi wa habari .
Surya Narayan Patro , msimamizi wa majanga , alisema kuwa "hakuna mtu ataruhusiwa kukaa katika nyumba za matope na nyasi katika maeneo ya pwani " wakati wa dhoruba.
Hadi jumamosi mchana, bahari ilikuwa tayari imesogea nchi kavu kama umbali wa mita 40 (130 futi ) kutikea sehemu za ukanda wa pwani.
" Naomba kila mtu asiwe na hofu, Tafadhali isaidieni serikali . . Kila mtu kuanzia kijiji hadi makao makuu wanatakiwa kuwa na tahadhari," aliwaambia waandishi wa habari .
Surya Narayan Patro , msimamizi wa majanga , alisema kuwa "hakuna mtu ataruhusiwa kukaa katika nyumba za matope na nyasi katika maeneo ya pwani " wakati wa dhoruba.
Hadi jumamosi mchana, bahari ilikuwa tayari imesogea nchi kavu kama umbali wa mita 40 (130 futi ) kutikea sehemu za ukanda wa pwani.
Maafisa sehemu zote mbili Orissa na Andhra Pradesh wamechukua
hatua za dharura kugawa chakula, vifaa na kuanzisha vituo vya kuhifadhi watu . Jeshi la India wameongeza nguvu juu ya hadhari
hiyo,wana malori , ndege na helikopta tayari kwa ajili ya shughuli za misaada.
No comments:
Post a Comment