WASHIRIKI wanaowakilisha nchi ya Tanzania katika mashindano ya Tusker Project Fame msimu wa sita yanayofanyika nchini Kenya wamenusurika kuingia kikaongoni wiki hii.
Washiriki hao walionusurika kuingia katika kikaango hicho ni Hisia, pamoja na Angel, ambapo wameonesha hali ya matumaini ya kuendelea kuwepo na kufanya vizuri katika mashindano hayo.
Washiriki walioingia katika kingao hiko ni pamoja na Fess (kenya), Jennifer (Kenya), Mishel (Kenya)Undercover Brother (Uganda), hali inayoonesha hati hati ya washiriki wa nchi ya Kenya.
Akielezea sababu ya washiriki hao kuingia katika kikaangoni 'Probation' jaji mwenye machachari Ian Mbugua alieleza kuwa shindano hilo halitafuti wasanii wa kawaida bali wenye vipaji na uwezo mkubwa zaidi Afrika Mashariki.
"Kwao hiyo ni changamoto kuingia ndani ya probation mashindano haya hatutafuti wasanii wa kawaida tu ,bali tunatafuta wasanii wenye uwezo mkubwa, hivyo ili kujitoa kikaangoni lazima waongeze juhudi" alisema Ian
No comments:
Post a Comment