Shule ya msingi Ilebula iliyopo Kata ya Kabungu Wilaya ya
Mpanda vijijini wametoa changamoto wanazo kabiliananazo katika mazingira ya
shule ikiwemo upungufu wa madarasa,madawati na nyumba za walimu.
Akiongea na Mpanda Fm Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Moses Mathias Makalawa amesema kuwa shule hiyo ina upungufu wa vyumba vya
madarasa ambapo shule nzima ina madarasa manne hali inayopelekea wanafunzi
kusomea chini ya mti na wengine katika ofisi za walimu.
Makalawa ameongeza kuwa shule hiyo ina wanafunzi
471 ambapo madawati katika shule nzima ni 39 ambayo hayakidhi idadi ya
wanafunzi na kupelekea wengine kukaa chini huku walimu wakiishi mbali na mahali
pa kazi kutokana na shule hiyo kumiliki nyumba mbili za walimu.
Hata hivyo mwalimu Makalawa ametoa wito kwa serikali
kutatua changamoto hizo ili kuongeza ufaulu katika shule hiyo na kufanikisha
mpango wa Big Result Now ulioanzishwa na serikali.
No comments:
Post a Comment