Wednesday, 23 October 2013

SERIKALI WILAYANI MPANDA MKOANI KATAVI IMESITISHA MKATABA WA MKANDARASI

by rahim kassonga (la Captain)

Serikali Wilayani Mpanda Mkoani Katavi imesitisha mkataba wa mkandarasi katika kijiji cha Itetemya Tarafa ya Karema kwa kushindwa kujenga  jengo la shule darasa 1 na ofisi 1 aliyokuwa amepewa ndani ya miezi 2 kuanzia mwezi Septemba  hadi Novemba na kupatiwa Mkandarasi mwingine ili kuendeleza ujenzi huo.
Mkandarasi huyo amenyanganywa tenda hiyo baada ya kushindwa kukamilisha ujenzi huo licha ya kuanza msingi na kushindwa kusimamisha ukuta kutokana na kuzidiwa tenda alizonazo.
Aidha Diwani wa Kata ya Karema Maiko Kapaka amethibitisha kusitishwa kwa mkataba huo na kusema kuwa tatizo la mkandarasi huyo kushindwa kuendeleza ujenzi ni kutokuwa na mtaji wa kutosha na Mkataba ulifanyika kati ya Makao Makuu ya Hifadhi ya Ziwa Tanganyika Mkoani Kigoma.
SOURCE:DAWATI
EDITOR:IRENE TEMU

No comments:

Post a Comment