Tuesday, 12 November 2013

PICHA;TIZAMA PICHA ZA UZINDUZI WA ALBUM YA MAKUHANI CHOIR JANA MAKANYAGIO

 by zangii ze icon
zangwinyo korobwinyo ....hatareee sana cheki nyomi mtu wangu

sema wewe....ni ful upako mpendwa....twende kazi
ilikuwa shangwe za ukweeee
ILIKUWA NI SIKU YA UZINDUZI WA ALBUM MPYA YA KWAYA HAPA MPANDA,


INAITWA MAKUHANI KWAYA,MGENI RASMI ALIKUWA MKURUGENZI WA RADIO MPANDA FM NA KWAKUWA ALIKUWA NJE YA NCHI KWA MATIBABU,ALIWAKILISHWA VEMA NA MENEJA KITUO GERLAD SETTY SEDEKIA 

AKIWA SAMBAMBA NA TEAM YA WAANDISHI WA HABARI MAHIRI TOKA 97.0 MPANDA FM SAUTI YA KATAVI 


RAHIM KASSONGA,BENEDICT KUZWA ,ALINANUSWE EDWARD NA TUNNU LUGOMBE AMBAYE ALIKUWA NDIYE MC WA SHUGHULI PALE KANISANI JIONEE PICHA HAPA
meneja kituo cha redio mpanda fm akikaribishwa na mchungaji na waumini kanisani


kwakutulia ....muite baba wawili ..kiroho safi  


mc tunu lugombe...bibi...amshaaaa popooo....
jambooo...makanyagioooo...haya nipo hapa kwa niaba mkurugenzi...amin mitha


mgeni rasmi...twakuomba uje uongee na wana katavi...huyu ndo mc bibi tunu

.....naahidi kwa niaba ya mkurugenzi wa mpanda fm..kutoa milioni mbili na nusu za ku shuti video yenu...pia promo kali ndani ya 97.0 voice of katavi....sedekia setty baba wawili



changizo likaendelea....



tuka pata risala kwa ufupi....



burudani.....




tuka maliza na kuondoka......


Thursday, 7 November 2013

Victoria Kimani amshambulia hater baada ya kumuita "Brainless Rihanna Copycut"


BY ZANGII ZE ICON
Mwanamuziki Victoria kimani, dada wa Rapper Bamboo ambae kwasasa anafanya vizuri na wimbo wake "Mtoto" amejikuta akipeleka majeshi kwa mtu mmoja ambae ni shabiki lakini ni hater ambae alithubutu kumwambia "hana akili"  kwa kuiga mavazi aliyokuwa ameyavaa Rihanna (Mexican Gangster) wakati wa haloween


Victoria Kimani kwenye haloween 2013


WASAMBAZAJI WAAKANDAMIZA WASANII WA FILAMU



WASANII wa filamu nchini bado wanaendelea kupokea  kipato kidogo kutoka kwa wasambazaji wa filamu hali iinayopelekea kudumaza  soko la filamu nchini, huku kupelekea wasanii hao kuwa na kipato cha chini.

Hayo yalibainishwa na msanii wa filamu za maigizo nchini Kulwa Kikumba 'Dude' ambapo aliweka wazi kuwa tasnia hiyo inaonekana kukuwa siku hadi siku ingawa wasanii hao bado wanaonekana kuwa masikini kutokana na kipato wanachopata.

Aliweka wazi kuwa mfumo mbaya wa mauzo ya filamu nchini ndio chanzo pekee kinachodidimiza kazi za wasanii hao huku baadhi yao wakikosa soko la filamu hali inayochangia baadhi yao kupotea katika tasnia hiyo.

Alibainisha kuwa wapo baadhi ya wasanii wanaendelea kunufaika kutokana na kazi zao lakini walio wengi wanaendelea kudidimia hadi hapo mfumo wa usambazaji utakapobadilika ndipo ahueni itakapopatikana kwa wasanii wengine.

" Sisi wasanii tumekosa ushirikiano kutokana na baadhi ya wasanii kunufaika na kazi hizo huku wengi kunyonywa na wasambazaji , ila kama tungeweza kushirikiana wasanii wote tukawa tunauza filamu kwa bei zinazolingana na ubora na ghrama ya filamu tungefika mbali" alibainisha Dude

LULU AKANUSHA KUCHUMBIWA


MSANII wa filamu nchini Elizabeth Michael 'Lulu' akanusha taalifa za kuzushiwa za kuchumbiwa na kukalibia kuolewa muda mchache zilizoandikwa na moja ya chombo cha habari jijini.

Lulu amekanusha taarifa hizo ambazo zimeandikwa na gazeti moja la udaku kuwa anatarajia kuolewa hivi karibuni  huku wazazi wake wakiwa tayari wameshapokea mahali.

Akizungumza na katika mahojiano , muigizaji huo ameweka wazi kuwa ameshangazwa na habari hizo ambapo baadhi ya magazeti mengi ya udaku ndiyo yamekuwa yakimwandika kile wanachojisikia.

Aliweka wazi kuwa hajachumbiwa na mwanaume yoyote yule na siku ikitokea amechumbiwa basi kila mtu atajua kwani halitakuwa jambo la kificho tena.

"Sijajua wao wameipata wapi hiyo habari kutoka chanzo kipi, kila kukicha kumekuwa na habari mtu akijisikia kuandika tu anaandika bila hata ya kufikiria leo wameandika nimechumbiwa, kesho wataandika nimeolewa, tena wataandika nimeachwa, kila watakalo lihisi kuandika wanaandika" alieleza Lulu.

Aliweka wazi kuwa kuchumbiwa kuolewa ni vitu ambavyo vimeumbiwa binadamu, vipo kama ukiwa na mpango wa mwenyezi mungu nitachumbiwa.

BAADA YA KUTOKA LUPANGO..... MASOGANGE APIGA ZA NUSU UTUPU

 SIKU chache baada ya kutoka lupango kwa msala wa madawa ya kulevya, ‘video queen grade one’ Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’ ametupia picha za utupu mtandaoni.
Agnes Gerald ‘Masogange’ katika pozi.
Masogange na mwenzake, Melisa Edward walikamatwa nchini Afrika Kusini Julai 5, mwaka huu wakidhaniwa kuwa na madawa haramu ya kulevya na baadaye mahakama kuu ya nchini humo ikawaachia kwa dhamana ikidai unga waliokutwa nao si madawa ya kulevya bali ni mali ghafi zijulikanazo kama Methamphetamine. Baada ya kuachiwa huru, Masogange anayesifika kwa kuwa na figa matata, alitupia picha hizo katika mtandao wa Instagram akiwa amevalia sidiria na nguo ya ndani pekee hali iliyowafanya wafuasi wa mtandao huo wamshangae huku wengi wakimlaumu kuwa alichokifanya hakifanani na maadili ya Mtanzania.
 
Video queen grade one Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’.
“Sasa huu upuuzi gani unatuwekea humu, kwani kila kitu unachofanya ni lazima sisi tuone? Hivi kwa nini mastaa wa Bongo wanapenda kujirahisi kiasi hiki?” alihoji mmoja wa wafuasi wa mtandao huo. Pamoja na wadau wengi kuonesha kukerwa na picha hizo, Masogange hakujali, aliwajibu kuwa kama hawataki kuziona picha hizo wamuondoe kwenye listi ya marafiki mtandaoni humo kwani siyo lazima. “Hii ni akaunti yangu, nina uhuru wa kuweka picha za aina yoyote. Kama mtu anaona nimemkera basi ‘aniblok’ maana hapa nimevaa mavazi ya kuogelea sasa mlitaka nivae pensi niogelee nayo? Simuogopi mtu…,” aliandika Masogange.

HII NI LAANA...!! MISS UTALII NA MSANII WA BONGO MOVIE WANASWA WAKISAGANA LIVE...CHEKI PICHA HAPA

Fathiya" Mrembo wa Facebook" na Suzi Magoti mshiriki kwenye filamua Ngema akimvua nguo mrembo huyo kuanza tendo.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida na kusikitisha matendo ya aibu kwa wasanii wetu yameendelea kushika kasi kama moto wa tipa baada ya blog hii makini kunasa picha nyingine za wasanii hawa wakusagana live bila chenga.
  Tumefanikiwa kupata picha hizi ambazo ni baadhi tu licha ya kwamba kuna CD nzima ya picha hizo tunazo kabatini na kuna taarifa kuwa pia kuna CD ya Viedo kabisa ambayo ndani yake kuna mambo ya kutisha.
tunakuahaidi siku mbili hizi itakuletea tuki hilo moja kwa moja kupitia blog hii pamoja na kuzimwaga picha hizo zaidi. Habari zaidi zilisema kuwa wasanii hao ambao mmoja alikuwa mshiriki Miss Utalii mwaka huu na mwingine ni staa kwenye filamu ya msanii Manaiki Sanga ambayo bado haijatoka na ndiye kwenye video hiyo anaonekana fundi wa kumbonyeza mwenzake.
Bofya hapo chini kuangalia picha hizo...




JINI KABULA ANYWA SUMU KISA PENZI LA CHUZ...

  Nyota wa Tamthiliya ya Jumba la Dhahabu, Miriam Nyafulwa Jolwa ‘Jini Kabula’ aliwahi kunywa sumu ambayo haikujulikana mara moja huku chanzo kikiwa ni ugomvi wa kimapenzi na mzazi mwenzake, Tuesday Kihangala ‘Chuz’. Akizungumza na mwandishi wetu mwanzoni mwa wiki hii, Chuz alisema tukio hilo lilijiri mwaka 2011 nyumbani kwake, Makongo jijini Dar na kwamba  siku hiyo hataisahau kutokana na jinsi alivyochanganyikiwa na hali ilivyokuwa. Aidha, Chuz alisema walikuwa na ugomvi mdogo tu wa kimapenzi jambo ambalo alitarajia kuwa lingeisha kwa amani. Lakini tofauti na matarajio yake, kila dakika iliyokuwa ikiondoka Kabula alizidi kupandisha mori kama si maruhani. Alisema muda mfupi baadaye, Jini Kabula  alivunja vioo vya gari lake kwa kutumia mawe kitendo kilichompa sababu Chuz kumpeleka polisi (hakutaja jina la kituo). Hata hivyo, Chuz aliendelea kushusha ‘vesi’ kuwa baada ya siku mbili, Jini Kabula alitolewa kwa dhamana huku yeye  akidhani kuwa yameisha lakini Kabula aliendeleza ‘libeneke’ ambapo alifika nyumbani  kwake na kujifungia ndani kisha akanywa dawa ambazo zilidaiwa kuwa ni sumu kali. “Nilipokuta mlango umefungwa nilianza kubisha hodi bila mafanikio. Niliamua kwenda polisi, wakaja na kuvunja mlango na kumkuta akiwa amelala chali huku akiwa anatokwa na povu jingi kinywani,” alisema Chuz.
Baadaye walimpa huduma ya kwanza kabla ya kumkimbiza hospitali (jina tunalo) kwa matibabu zaidi. Hata hivyo, baada ya kutibiwa, Chuz aliomba yaishe kwa amani.
“Kaka sitaisahau siku hiyo, ilikuwa  mbaya sana kwangu. Jini Kabula alikuwa kabadilika kabisa, alidhamiria kujiua kweli. “Nashukuru hamkupata habari hiyo lakini ilinichanganya sana,” alisema Chuz.
Mwandishi alimtafuta Jini Kabula kwa njia ya simu ili kuthibitisha juu ya habari hizo ambapo baada ya kusomewa madai hayo alianza kwa kucheka na kujibu:
“Duh! Wewe ni kiboko, umezipata wapi hizo habari? Lakini sipendi kuzungumzia mambo ya zamani, muulize vizuri aliyekwambia.”

HUU NDO UJANJA WA DIAMOND NA UZEMBE WA ALI KIBA ..

Hata kama sio shabiki wa diamond ila kuna kitu lazima uwe kinakuvutia kutoka kwake.Unaweza kujitahidi kumchukia labda kutokana na skendo zake za nje ya muziki wake ila ukirudi kwenye muziki wake nadhani anastahili kuwa pale alipo.
Kuanzia muonekane wake mpaka anavyoweza kuji-brand kimataifa na anavyojua kucheza na akili za mashabiki.

Wasanii wengi wa bongo flava wana tabia ya kurithika kwa mafanikio yao ila Diamond toka atoke na Kamwambie mwaka 2009 mpaka 2013 amezidi kwenda juu bila kuonyesha kusuasua wala kutetereka.
Angalia video ya number 1.Wimbo unaweza sema ni wa kawaida kabisa ukilinganisha na mbagala, kamwambie au nitarejea ila akili ya kwenda kufanya video cape town,south africa kumeifanya nyimbo iwe number 1 kama jina lake lilivyo.

Ushawahi kujiuliza Ali kiba yupo wapi pamoja na kuwa kila mtu anajua ni mkali kuliko diamond?Ali kiba toka atoe my everything mwisho wa mwaka jana amepotea hata video ajatoa.Tukaja kumuona kwenye kidela na Abdu kiba bila kurefusha maneno Ali anashindwa kuufanya mziki wake kama mashabiki wake wanavyotarajia labda pengine angekuwa anafukuzana na diamond ila matokeo yake vijana wake kama Rich mavoko na Dimpoz ndio wapo nyuma ya Diamond huku Ali akibaki msanii mkali ambae ameshindwa kuendelea kutuonyesha ukali wake sijui anawaza nini!

Ushawahi kujiuliza kama ule wimbo wa airtel hands across the world waliopiga wakina r.kelly,fall ipupa,2 face kama nafac ile angeipata diamond leo angekuwa wapi?
Diamond leo anatuletea remix ya number 1 f.t Davido kila mtu anaisubiri kwa hamu ila Ali alishindwa hata kutuletea remix ya Dushelele f.t Fally ipupa pamoja kukaa nae wiki nzima wakifanya wimbo pamoja.
Diamond ni mjanja anaejua biashara ya mziki ilivyo labda pengine ni management yake inayomsimamia.Diamond kaweza kuubadilia mziki wetu kwa kiasi chake leo ndio msanii anaelipwa pesa nyingi kwa show.

Nampenda ali kiba,naipenda sauti yake,anajua mziki kuliko Diamond ila Ali ameshindwa kubadilika na kukubali soko la mziki linataka nini.

Amka Ali huyu Diamond hakuwezi ila usipokuwa makini utajikuta nyuma ya rich,barnaba,dimpoz na ben pol maana mziki sio kuimba peke yake mziki ni biashara pia

Monday, 4 November 2013

Kesi dhidi ya Morsi kuanza leo Misri

by rahim kassonga (La Captain)

Wameshitakiwa kwa kosa la kuchochea mauaji ya waandamanaji wakati wa vurugu za kisiasa nje ya ikulu ya Rais mwezi Disemba mwaka jana.
Vikosi vya usalama vimedhibiti hali ya usalama baada ya wafuasi wa Morsi kuitishia kufanya maandamano makubwa.
Morsi aliondolewa uongozini kwa nguvu za jeshi mwezi Julai baada ya maandamano ya kila mara kufanyika kupinga utawala wake.
Rais aliyeng’olewa mamlakani nchini Misri, Mohammed Morsi anatarajiwa kufikishwa mahakamani leo pamoja na vigogo wengine 14 wa chama cha Muslim Brotherhood, wakati kesi yake itakapoanza kusikilizwa mjini Cairo.
Ingawa alishinda urais kwa njia ya demokrasia, wakati wa uongozi wake wa zaidi ya mwaka mmoja, Morsi hakuelewana sana na taasisi nyingi za serikali.
Baada ya kupinduliwa na jeshi, maandamano yalifanyika kila kulipokucha mjini Cairo na makubwa zaidi yalikuwa ya wafuasi wake kukesha karibu na kasri la rais wakitaka Morsi aachiliwe.
Polisi walaisababisha mamia ya vifo vya wafuasi hao walipovunja maandamano yao kwa nguvu.
Serikali ya muda pia imekuwa ikiwasawa na kuwakamata wanachama wa Muslim Brotherhood, chama chake Morsi.
Serikali pia imeharamisha vyama vyote vya kisiasa huku ikiwakamata mamia ya viongozi wa mashirika hayo.
Wafuasi wake wanasema kuwa alipinduliwa na jeshi na sasa anakabiliwa na kesi ya kisiasa.
Mashirika ya kutetea haki za binadamu, yameituhumu maafisa wa usalama kwa kufanya kazi yao bila uwajibikaji.


Sunday, 3 November 2013

Mourinho kimyaa abamizwa na Newcastle 2 - 0


Newcastle wakiwa katika uwanja wao nyumbani wa St. James Park jumamosi hii wameisambaratisha Chelsea kwa jumla ya magoli 2 -0 katika mechi ya ligi kuu ya England.

Newcastle walianza kusherekea ushindi baada ya kupata goli la kuongoza katika dakika ya 67 lililofungwa kwa kichwa cha kuchumpa na Yoan Gouffran.
Wakicheza kwa kujiamini Loic Remmy wa Newcastle alizidi kupigilia mwiba mkali kwa mashabiki wa Chelsea pale alipopachika goli la pili katika dakika 89.
Kwa matokeo hayo Newcastle sasa itakuwa na point 14 huku na Chelsea ikibakiwa na pointi 20.