Thursday 7 November 2013

WASAMBAZAJI WAAKANDAMIZA WASANII WA FILAMU



WASANII wa filamu nchini bado wanaendelea kupokea  kipato kidogo kutoka kwa wasambazaji wa filamu hali iinayopelekea kudumaza  soko la filamu nchini, huku kupelekea wasanii hao kuwa na kipato cha chini.

Hayo yalibainishwa na msanii wa filamu za maigizo nchini Kulwa Kikumba 'Dude' ambapo aliweka wazi kuwa tasnia hiyo inaonekana kukuwa siku hadi siku ingawa wasanii hao bado wanaonekana kuwa masikini kutokana na kipato wanachopata.

Aliweka wazi kuwa mfumo mbaya wa mauzo ya filamu nchini ndio chanzo pekee kinachodidimiza kazi za wasanii hao huku baadhi yao wakikosa soko la filamu hali inayochangia baadhi yao kupotea katika tasnia hiyo.

Alibainisha kuwa wapo baadhi ya wasanii wanaendelea kunufaika kutokana na kazi zao lakini walio wengi wanaendelea kudidimia hadi hapo mfumo wa usambazaji utakapobadilika ndipo ahueni itakapopatikana kwa wasanii wengine.

" Sisi wasanii tumekosa ushirikiano kutokana na baadhi ya wasanii kunufaika na kazi hizo huku wengi kunyonywa na wasambazaji , ila kama tungeweza kushirikiana wasanii wote tukawa tunauza filamu kwa bei zinazolingana na ubora na ghrama ya filamu tungefika mbali" alibainisha Dude

No comments:

Post a Comment