Monday 4 November 2013

Kesi dhidi ya Morsi kuanza leo Misri

by rahim kassonga (La Captain)

Wameshitakiwa kwa kosa la kuchochea mauaji ya waandamanaji wakati wa vurugu za kisiasa nje ya ikulu ya Rais mwezi Disemba mwaka jana.
Vikosi vya usalama vimedhibiti hali ya usalama baada ya wafuasi wa Morsi kuitishia kufanya maandamano makubwa.
Morsi aliondolewa uongozini kwa nguvu za jeshi mwezi Julai baada ya maandamano ya kila mara kufanyika kupinga utawala wake.
Rais aliyeng’olewa mamlakani nchini Misri, Mohammed Morsi anatarajiwa kufikishwa mahakamani leo pamoja na vigogo wengine 14 wa chama cha Muslim Brotherhood, wakati kesi yake itakapoanza kusikilizwa mjini Cairo.
Ingawa alishinda urais kwa njia ya demokrasia, wakati wa uongozi wake wa zaidi ya mwaka mmoja, Morsi hakuelewana sana na taasisi nyingi za serikali.
Baada ya kupinduliwa na jeshi, maandamano yalifanyika kila kulipokucha mjini Cairo na makubwa zaidi yalikuwa ya wafuasi wake kukesha karibu na kasri la rais wakitaka Morsi aachiliwe.
Polisi walaisababisha mamia ya vifo vya wafuasi hao walipovunja maandamano yao kwa nguvu.
Serikali ya muda pia imekuwa ikiwasawa na kuwakamata wanachama wa Muslim Brotherhood, chama chake Morsi.
Serikali pia imeharamisha vyama vyote vya kisiasa huku ikiwakamata mamia ya viongozi wa mashirika hayo.
Wafuasi wake wanasema kuwa alipinduliwa na jeshi na sasa anakabiliwa na kesi ya kisiasa.
Mashirika ya kutetea haki za binadamu, yameituhumu maafisa wa usalama kwa kufanya kazi yao bila uwajibikaji.


No comments:

Post a Comment