Thursday 28 November 2013

WAZEE KATAVI WASHAURI SERIKALI KUENDELEA NA OPERESHENI TOKOMEZA UJANGILI




MWAMLIMA-DC

Wazee Mkoani Katavi wameshauri Serikali kuendelea na operation tokomeza ujangili kwa kuwa imesadia kwa kiasi kikubwa kuokoa rasilimali za Taifa zilizokuwa zikiteketea kutokana na baadhi ya watu wachache waliokuwa wakijihusisha na ujangili wa kuhujumu rasilimali hizo.
Wakiongea kwenye Mkutano Maalum wa majadiliano na Wazee wakiwa na  Mkuu wa Wilaya Mpanda Paza Mwamlima  wamezungumzia  juu ya wahamiaji haramu nao wanajihususha kwa njia moja au nyingine na   katika vitendo vya ujangili na uharibifu wa mazingira wamesema hali hiyo ikiendelea uharibifu wa rasilimali za Taifa kama wanyama pori na mistu,  na  uharibifu wa mazingira hali inayoashiria    kutoweka  kwa  rasilimali  za taifa.

Kwa upande wake Mkuu huyo wa Wilaya  ya Mpanda Paza Mwamlima amesema katika   operation tokomeza  ujangili iliyofanyika Mkoani  Katavi  katika Wilaya ya Mpanda  Kata  moja  ya Mwese pekee jumla ya silaha 250 zilikamatwa hiyo inaonesha ni namna gani watu wanaishi na silaha ambazo hutumika kwa vitendo vya ujangili hivyo amewaomba wazee hao kusaidia kwa njia moja au nyingine kuwafichua watu wa namna hiyo wanaojihusisha na  uharifu, akaongeza  kuwa wazee ni tunu ya Taifa na amani katika nchi Wazee wanasaidia katika kuimarisha amani.
Awali katika risala yao wazee walimweleza Mkuu wa Wilaya kuwa wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa usafiri wa kuwafikia wenzao walioko mbali kutoka makao makuu ya wilaya na Mkoa kuwafikia wazee wenzao walioko wilaya ya Mlele na Kata za Inyonga, mamba. Majimoto, kasansa kibaoni ,usevya mwamapuli,mbede,ikuba, Nsenkwa, Ilelea, Ilunde na Utende
Pia alitaja wazee wengine walioko katika kata za mwese, karema ,ikola,  Mishamo katuma Kapalamsenga na sibwesa pamoja  na maeneo mengine imekuwa tatizo kuwafikia hivyo wanaomba kusaidiwa kutatua changamotohiyo.
Changamoto nyingine waliyozungumzia  ni wazee kutohudumiwa ipasavyo hususani wanpokuwa wakipatiwa matibabu katika Hospitali wakaeleza kuwa wanakumbana na vikwazo vingi,pia wakaomba kusamehewa na mambo mengine kama kulipia umeme na huduma nyingine.
Mmoja wa wazee aliyejitambulisha kwa jina la John Kisalala aliomba eneo la kusaidia wazee matibabu liwekewe utaratibu mzuri ili kuondoa usumbufu kwa wazee hao ikiwa ni pamoja na kuondolewa usumbufu wa kulipia huduma ya maji, umeme na huduma nyingine kwa kuwa wazee hao wamelitumika taifa kwa muda mrefu na sana na sasa wanatakiwa kuhudumiwa.
Akizungumzia operation tokomeza ujangilia na operation kimbunga wazee hao wameshauri washirikishwe katika zoezi hilo kwa kuwa wazee wanawatambua watu ambao sio wazawa wao wanawatambua watu ambao siyo raia halali.
Naye Benezite Mwanauta akizungumzia uharibifu wa mazingira na rasilimali za taifa amewalaumu wafungaji wa kabilia la kisukuma kwa kukataa miti hovyo huku watu waliopewa dhamana wakiwa wanaangali bila kuchukua hatua yeyote  huku mazingira yakiendelea kuharibika suala hilo lisipochukuliwa hatua na umuhimu wa kipeke huenda katavi ikageuka jangwa walishauri hatua za makusudi zichukuliwe ili kunusuru uharibifu huo.
sikiliza hapa
http://www.hulkshare.com/356bxvkxsp1c

No comments:

Post a Comment