Friday 25 October 2013

Msanii wa bongo movie anusurika kuliwa KIBOGA.....Alizidisha pombe na kujikuta chooni akiwa mtupu.





Muigizaji wa filamu za kibongo anayejulikana kwa jina la Danny Cloud  maarufu  kama  Danny mtoto wa mama  ambaye  alipata  umaarufu  wa  jina  hilo  kupitia  filamu ya mtoto wa mama  amenusurika  kubakwa ( kuliwa kiboga ) 

Akizungumza  na  mpanda fm, rafiki wa karibu wa msanii huyo  alidai kwamba  Danny  alikuwa maeneo ya Bilcanas  ambapo  alipewa  ofa  ya  pombe  na  jamaa  zake...

Rafiki huyo  alidai  kuwa, baada  ya  kupewa  ofa  hiyo  adimu, msanii  huyo  alianza  kuiparamia  pombe mfano  wa  mtu  mwenye  kiu  kali  ya  maji, hali  iliyomfanya  asijitambue  na  kuanza  kuvua  nguo...

"Kuna  wakati Danny  alinyanyuka  na  kuelea  chooni  huku  akipepesuka...Alipofika  huko  alidondoka  na kulala  huko huko chooni, hali  iliyowafanya   vibaka  watake  kumla  kiboga"...Alisema  huyo rafiki  yake  na  kuongeza:

"Baada  ya  kimya  kirefu, ilibidi  tukamwangalie  ambapo  tuliwakurupusha  vijana  watatu  wakiwa  wameshamvua  nguo"

No comments:

Post a Comment