Monday 28 October 2013

tutatumia umeme wa gesi asilia na makaa ya mawe;Prof.Sospeter Muhongo

by rahim kassonga (La Captain)



Waziri wa Nishati na madini Pr.Sospeter Muhongo  amesema Serikali imedhamiria kutumia gesi asili na makaa ya mawe pamoja na vyanzo vingine vya kuzalisha umeme ili kuwawezesha wananchi zaidi ya asilimia 30 kutumia Nishati hiyo ya umeme ifikapo mwaka 2015.

Akiwa Mjini Mpanda katika siku yake ya kwanza ya kukagua utekelezaji wa mradi wa umeme katika maeneo ya vijijini kwa kiwango cha zaidi ya asilimia 10 toka asilimia chini ya 7 za sasa ambapo Pr.Muhongo amesema lengo la wananchi kukabiliana na tatizo la umaskini ifikapo mwaka 2025 haliwezi kukamilika ikiwa Nishati ya umeme haitazalishwa kwa wingi.

Akizungumza na Viongozi wa Serikali wa Mkoa wa Katavi Pr.Muhongo amesema kuwa kwa kutambua umuhimu wa Nishati ya umeme kwa maendeleo ya Taifa na ukuzaji wa uchumi kwa mtu mmoja mmoja Serikali imeweka nia ya kweli kuhakikisha uzalishaji wa Nishati hii muhimu unaongezeka.


Taarifa ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mh.Rajabu Lutengwe imeeleza mikakati ya Serikali Mkoani humu kushirikiana na wakala wa mradi wa kusambaza umeme vijijini ambapo kiasi cha shilingi bilioni 10 zitatumika kusambaza umeme katika vijiji 14.

No comments:

Post a Comment