Sunday 13 October 2013

MAAFA YAIKUMBA INDIA, MAELFU WAHAMA MAKAZI YAO


by rahim kassonga


BEHRAMPUR , India
Dhoruba kubwa imeikumba nchi ya India kufuatia mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali (kimbunga) kunyesha kwenye  ukanda wa pwani ya mashariki ya India jumamosi jioni na kuleta uharibifu mkubwa wa makazi ya watu huku maelfu wakiyahama makazi yao na kutafuta hifadhi salama
wimbi kubwa likielekea pwani kwenye bandari ya Jalaripeta kwenye wilaya ya Visakhapatnam kusini mwa nchi ya India na kuharibu makazi zaidi ya 10,000

Barabara zote zilikukuwa tupu wakati mawimbi makubwa yalipoingia kwenye mwambao wa mji wa Orissa , ambao ulikumbwa na Kimbunga kikali. Jumamosi mchana. 
wanakijiji walioathiriwa na kimbunga, wakipata chakula katika hifadhi ya muda huko Chatrapur kilometa 200
Upepo mkali uliotishia hata wanaume watu wazima ulivuma kwenye mji huo. Maji ya bahari yalisukumwa kuelekea nchi kavu na kukumba vijiji vilivyokaliwa na wakulima wadogowadogo vyenye vibanda vya matope na nyasi.
wake wa wavuvi wa india wakiwaashiria waume zao (wavuvi) kurudi kufuatia dalili za kimbuka
Wakati kimbunga kikivumba kwenye mwambao wa Bengal kuelekea pwani ya Hindi, picha za  satellite zinaonyesha kimbuka hicho kinazunguka na kiini chake kufunika eneo lenye ukubwa zaidi ya Ufaransa. Picha zilionesha kuwa dhoruba kubwa ingelikumba pwani ya Gopalpur mapema jumamosi usiku
mwamvuli haukufaa kwa upepo mkali

Ikiwa na eneo kubwa lenye maji ya moto duniani, Bahari ya Hindi inachukuliwa kama chanzo cha dhoruba na baadhi ya dhoruba zilizoleta maafa makubwa kwenye siku za karibuni ilitokea kwenye pwani ya Bengal, ikiwa ni pamoja na kimbunga cha mwaka 1999 ambacho pia kiliikumba Orissa na kuua watu 10,000.
familia ikibebelea mizigo yao na kuelekea sehemu salama

Viongozi wa serikali wanasema idadi kamili ya vifo haijajulikana na itawekwa wazi siku ya jumapili.

Katika mji wa Behrampur , kilometa 10 ( maili 7 ) toka eneo la bara ambapo dhoruba ndio ilikuwa imelenga, anga liliingia giza ghafla wakati dhoruba hilo lilipotua likiwa na upepo mkali iliyoambatana na mvua nzito na kuacha mitaa yote ya mji huo ikiwa mitupu .
waathiriki wa dhoruba hiyo wakipata chakula kwenye hifadhi ya muda


Madirisha ya nyumba yalipasuka kutokana na upepo mkali. Huku vitu vya zilivyokuwa nje ya nyumba vikisikika kugonga kuta za nyumba.

"Wazazi wangu wamekuwa wakinipigia simu mara kwa mara ... walikuwa na wasiwasi sana ," alisema HEMANT PATI , 27, ambaye alikuwa kujificha katika hoteli na watu wengine 15 kutoka mji wa pwani ambao ulikuwa wa kwanza kukumbwa na dhoruba.

wanakijiji walijilinda na mvua kubwa kwa kujifunika na manailoni
Meneja wa hoteli hiyo alisema alifunga milango dhidi ya mtu yeyote kujaribu kuingia , akisema kulikuwa na chakula, maji na umeme wa jenereta tu kwa ajili ya wageni ya Jyoti Hoteli. "Hakuna mtu anaweza kuja ndani , na hakuna mtu anaweza kwenda nje," Shaik Nisaruddin alisema.

wanaume wakijarinu kuutoa mti ulioanguka barabarani kufuatia mvua na upepo mkali octoba 12
Makadirio ya nguvu ya dhoruba imeshuka kidogo,kulinganisha na taarifa ya onyo iliyotolewa na Jeshi la Maji la Marekani pamoja na kituo cha tahadhari (Typhoon Warning Centre) jijini Hawaii iliyoonyesha uwepo upepo endelevu wenye kasi ya kilomita 222 kwa saa ( 138 maili kwa saa ), na kupanda hadi 268 km/h (167  mph).

wanakijiji wa india wakipambana na upepo mkali
Ingawa dhoruba, iliendelea kuwa na nguvu nyingi mno na hatari. Saa chache kabla ya kugonga ardhi , kiini cha dhoruba hiyo kilitawanyika na kueneza upepo mkali kwenye maeneo mengi zaidi na kusababisha madhara makubwa ," alisema Jeff Masters, mkurugenzi wa hali ya hewa katika kituo binafsi cha hali ya hewa kilicho chini ya Marekani
msichana akichungulia dirishani akiwa anasafiri kwa basi kuelekea eneo salama
" Ni kitu kibaya pale kilipotua  kwenye nchi kavu, nyumba nyingi nchini India haziwezi kuhimili hata dhoruba dhaifu " Masters alisema.
Pia alisema si pwani pekee itapata uharibifu mkubwa. "Hii ni dhoruba yenye nguvu na yakushangaza, itabeba upepo wa kimbunga kuupeleka bara kwa muda wa takribani masaa 12, ambayo si kawaida kabisa  , " alisema Masters kabla ya kutokea kwa dhoruba hiyo.


Vimbunga kawaida kupoteza nguvu vinapopiga nchi kavu, ambapo kuna unyevu wenye joto dogo ambao huuathiri nishati nguvu ya dhoruba.
Ijumaa jioni, baadhi ya watu zaidi ya 420,000 walihama makazi yao kuelekea kwenye hifadhi na ardhi ya juu katika mji wa Orissa, na 100,000 zaidi katika mji jirani wa Andhra Pradesh , alisema Anil Goswami katibu wa mambo ya ndani ya Indaia.
L.S. Rathore , mkuu wa Idara ya Hali ya Hewa ya Hindi , alitabiri kuongezeka dhoruba kwa kipimo cha mita 3-3.5 ( 10-11.5 futi) , lakini watalaam kadhaa  wa Marekani walitabiri dhoruba kubwa sana ya maji na kuelekea pwani . Ryan Maue mtaalatam wa hali ya hewa toka shirika binafsi la Marekani (Weather Bell) alisema kuwa, hata katika mazingira bora, ubashiri ulionesha  kutakuwa na mawimbi ya mita 7-9 (20-30 futi).
Kuongezeka kwa dhoruba ni muuaji makubwa katika dhoruba kama ile, ingawa mvua kubwa ilichangia kuzidisha uharibifu. Serikali ya India imeisema watu milioni 12 wataathiriwa na dhoruba, ikiwa ni pamoja na mamilioni wanaoishi mbali na pwani.
Kulikuwa na taarifa chache za dhoruba huko  Orissa muda mchache baada ya dhoruba kuanza kupiga, kwa Phailin tayari kulikuwa na dhoruba kubwa kwa karibu masaa 36, na upepo mkubwa kuongezeka, alisema Maue. "Dhoruba hii kubwa haiwezi kumalizima haraka, " alisema.


Kimbunga cha mwaka 1999 kilikuwa na nguvu kama hiki cha Phailin lakini kilifunika eneo ndogo - kilirusha nje kama mita 5.9 (19.4 -futi).
Masaa kadhaa kabla ya dhoruba hii , wanakijiji wapatao 200 walikusanyika kwenye vyumba viwili, kwenye nyumba imara ya seruji shuleni katika kijiji cha Subalaya , umbali wa kilomita 30 ( maili 20 ) kutoka pwani , wakati maafisa wa mambo ya dharura ya ndani wakisambaza chakula na maji. Barabara zote zilikuwa karibu tupu, ila kwa ajili ya malori mawili kuleta misaada zaidi kwenye shule hiyo. Watoto walionekana kutetemeka na kutereza katika mvua wakiwa wanashushwa kutoka kwenye malori, wakiwafuata wanawake waliokuwa wamebeba mizigo

Wengi wenye makazi ya chini walikimbilia kwenye hifadhi , lakini baadhi yao walibaki na jamaa zao wakihofia dhoruba inaweza kuwakumba wakiwa njiani.

"Mtoto wangu alibaki na mke wake kwa sababu ya ng’ombe na mali ," alisema Kaushalya Jena mzee wa miaka 70 akilia kwa hofu ndani ya makazi ya muda. "Mimi sijui kama wao ni salama. "
Huko Bhubaneshwar na katikati ya mji wa Orissa, maafisa wa serikali na kujitolea kwa pamoja  waliweka maelfu ya mifuko ya chakula kwa ajili ya makambi ya misaada.

"Inaonekana ajabu, kwa sababu siku ilikuwa ni nzuri na jua lilikuwepo ," alisema Doris Lang wa Honolulu , ambaye alikuwa na rafiki katika mahekalu kando ya bahari kwenye mji wa Puri wakati habari za kimbunga zilipowafikia wao.
Kiongozi wa juu wa serikali, Waziri Kiongozi Naveen Patnaik , amewaasa watu kuwa watulivu .

" Naomba kila mtu  asiwe na hofu, Tafadhali isaidieni serikali . . Kila mtu kuanzia kijiji hadi makao makuu wanatakiwa kuwa na tahadhari," aliwaambia waandishi wa habari .

Surya Narayan Patro , msimamizi wa majanga , alisema kuwa "hakuna mtu ataruhusiwa kukaa katika nyumba za matope na nyasi  katika maeneo ya pwani " wakati wa dhoruba.

Hadi jumamosi mchana, bahari ilikuwa tayari imesogea nchi kavu kama umbali wa mita 40 (130 futi ) kutikea sehemu za ukanda wa pwani.






Maafisa sehemu zote mbili Orissa na Andhra Pradesh wamechukua hatua za dharura kugawa chakula, vifaa na kuanzisha vituo vya kuhifadhi watu .  Jeshi la India wameongeza nguvu juu ya hadhari hiyo,wana malori , ndege na helikopta tayari kwa ajili ya shughuli za misaada.



No comments:

Post a Comment