Monday 28 October 2013

VIWANJA MISUNKUMILO

by rahim kassonga (La Captain)


Wananchi wa Kata ya Misunkumilo Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi wameulalamikia Uongozi wa Kata yao kwa kushindwa kufuatilia viwanja walivyo takiwa kugawiwa na Idara ya Ardhi.

Wananchi hao wamesema kuwa Augosti mwaka huu Idara ya Ardhi ilifanya tathmini ya  viwanja kwa ajili ya kupanga mpangilio maalumu wa kuacha nafasi ya barabara za Mitaa lakini mpaka sasa hawajarudi kwajili ya kugawa viwanja hivyo.

Aidha wananchi hao wamesema kuwa kutokana na kufuatilia na kukaa kwa muda mrefu baadhi ya wananchi wameanza kujenga ili waweze kuishi katika nyumba zao kwasababu wamechoka kukaa kwenye nyumba za kupanga.

Hata hivyo Mtendaji wa Kata hiyo January Kayungilo amesema kuwa Idara ya Ardhi imeshafanya tathmini, hiyo amewaomba wananchi  kusubiri shughuli ya kuanza kugawa viwanja hivyo kwaajili ya kuvilipia ili waweze kujenga nyumba zao pia amewataka wananchi hao kuwa wavumilivu katika suala hilo.

EDITOR:TIDA SAIDEA

No comments:

Post a Comment