Friday 25 October 2013

MAJANGA KWENYE ELIMU, WANAFUNZI 471, MADAWATI 39, MADARASA 4, WAPI SERIKALIII !!!!!

by rahim kassonga (La Captain)


Shule ya msingi Ilebula iliyopo Kata ya Kabungu Wilaya ya Mpanda vijijini wametoa changamoto wanazo kabiliananazo katika mazingira ya shule ikiwemo upungufu wa madarasa,madawati na nyumba za walimu.

Akiongea na Mpanda Fm Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Moses Mathias Makalawa amesema kuwa shule hiyo ina upungufu wa vyumba vya madarasa ambapo shule nzima ina madarasa manne hali inayopelekea wanafunzi kusomea chini ya mti na wengine katika ofisi za walimu.

Makalawa ameongeza kuwa shule hiyo ina wanafunzi 471 ambapo madawati katika shule nzima ni 39 ambayo hayakidhi idadi ya wanafunzi na kupelekea wengine kukaa chini huku walimu wakiishi mbali na mahali pa kazi kutokana na shule hiyo kumiliki nyumba mbili za walimu.

Hata hivyo  mwalimu Makalawa ametoa wito kwa serikali kutatua changamoto hizo ili kuongeza ufaulu katika shule hiyo na kufanikisha mpango wa Big Result Now ulioanzishwa na serikali.




No comments:

Post a Comment