Ni
Sunday, 28 September 2014
VAN GAAL ASEMA WACHEZAJI WAKE WANAJARIBU
Maneja wa kilabu ya Manchester United Van Gaal katikati.
Mkufunzi wa kilabu ya Manchester United Louis Van Gaal amekiri kwamba wachezaji wa timu hiyo wanajitahidi kuelewa mbinu zake.
Mkufunzi huyo wa Uholanzi anasimia kilabu hiyo ikiwa na matokea mabaya zaidi tangu msimu wa ligi ya Uingereza uanze,huku ikiwa imejipatia pointi tano pekee kwa mechi tano ilizocheza.
Wikendi hii timu hiyo inatarajwa kupambana na timu ya West Ham.''tunawapatia wachezaji mafunzo mengi '',Van Gaal alinukuliwa akisema.
''Itafikia wakati katika msimu huu ambapo mafunzo tunayotoa yatakuwa si mengi''.
Wakati huu pengine mafunzo hayo mengi mno.
Tangu achukue usimamizi wa timu hiyo mnamo mwezi July tarehe 16,Van Gaal ametumia mbinu tofauti katika timu hiyo mbali na mabadiliko kadhaa katika mtindo wake wa ukufunzi ili kujaribu kuweka filosofia yake.
Kocha huyo aliyewahi kuifunza Ajax,Barcelona na Bayern Munich ana imani kwamba kilabu hiyo itafaidika lakini amekiri kwamba huenda aliwasukuma sana na kwa haraka wachezaji hao kujifunza mbinu mpya.
SERIKALI YANG'AKA KITENDO CHA KUYAFUNGIA MAGAZETI.
Juma Nkamia, Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Serikali imesema haina mpango wa kuvifungia vyombo vya habari yakiwamo magazeti badala yake itaendelea kuvionya vinavyokiuka maadili.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia, alisema hayo jana kufuatia gazeti la NIPASHE kuandikiwa barua na ofisi ya Msajili wa Magazeti, kutaka lijieleze baada ya kuchapicha habari kuhusu Bunge la Katiba jinsi linavyotumia mabilioni ya fedha.
Akizungumza katika kipindi cha Jambo Tanzania kinachorushwa na TBC akiwa mjini Dodoma, alisema siyo nia ya serikali kuyafungia magazeti isipokuwa yanapokiuka taratibu yataonywa.
Hata hivyo, Nkamia alikaririwa hivi karibuni akisema serikali inajiandaa kuyachukulia hatua kali baadhi ya magazeti kwa madai kwamba yamekiuka maadili na kutishia usalama wa nchi,
Nkamia, alikaririwa kuyasema hayo aliposhiriki hafla ya uzinduzi wa nembo mpya ya kituo cha Redio Tripple A cha jijini Arusha, na kuwa utekelezaji wa azma hiyo hautajali mmiliki wa chombo husika.
Sababu iliyodaiwa kutolewa na Nkamia dhidi ya magazeti hayo ambayo hata hivyo hakuyataja, ni kwamba kuandika habari za uchochezi.
Lakini katika mahojiano ya jana, Nkamia akasema “siyo dhamira ya serikali kuyafungia magazeti, magazeti haya yameajiri vijana wengi ambao hawana kazi, lakini yanapokiuka utaratibu tunaitana tunarekebishana tu, sidhani kama serikali itafanya hivyo,” alisema.
Alisema habari iliyochapishwa na NIPASHE kwamba fedha zinazotumika katika Bunge la Katiba zinaweza kupangwa kutoka Dar es Salaam hadi Bukoba kimsingi halikuwa jambo zuri.
Hivi karibuni serikali ilimwandikia barua Mhariri Mtendaji wa NIPASHE kumtaka ajieleze kuhusiana na habari zilizochapishwa Septemba 15, mwaka huu kuhusu Bunge la Katiba.
Katika barua hiyo ya Septemba 16, mwaka huu kutoka Wizara ya Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo, iliyotiwa saini na Raphael Hokororo, kwa niaba ya Msajili wa Magazeti ilieleza kuwa gazeti hilo lilichapisha habari za uchochezi ambazo zinajenga hisia mbaya kwa wananchi juu ya serikali yao kuhusu bunge hilo.
Majambazi wapora milioni 30.6 wajeruhi Polisi, Mfanyabiashara
WATU wawili akiwamo askari mmoja wamenusurika kifo baada ya kupigwa risasi na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi, waliofanikiwa kupora mfuko wa fedha unaosadikiwa kuwa na zaidi ya shilingi milioni 30.
Sajenti Hija Hassan Hija, alijaribu kupambana na mabambazi hao, lakini alishindwa kufanikiwa baada na yeye kujeruhiwa sehemu ya mkononi na mguuni kutokana kushambuliwa kwa risasi.Akiwa katika hospitali ya Mnazi mmoja akjipata huduma ya kwanza.
Tukio hilo, lilitokea jana mchana majira ya 8:30 katika Mtaaa wa Mlandege Mkoa wa Mjini Magharibi, ambapo majambazi hao walimvamia mmoja wa wafanya biashara wa Mchele hapa nchini aliyetambulika kwa jina la Salum Issa Suleiman (50), Mkaazi wa Baghani Mjini Unguja ,, ambaye walimpora mfuko wake wa fedha hizo wakati akiwa njiani kuzipeleka benki.
Tukio hilo, lilitokea jana mchana majira ya 8:30 katika Mtaaa wa Mlandege Mkoa wa Mjini Magharibi, ambapo majambazi hao walimvamia mmoja wa wafanya biashara wa Mchele hapa nchini aliyetambulika kwa jina la Salum Issa Suleiman (50), Mkaazi wa Baghani Mjini Unguja ,, ambaye walimpora mfuko wake wa fedha hizo wakati akiwa njiani kuzipeleka benki.
Mfanyabiashara wakati akiwa njiani alijikuta akizingirwa na mojaya gari ndogo na kuanzakushambuliwa kwa risasi ambazo zilimjeruhi sehemu zake za miguuni na ghafla kuanguka na ndipo majambazi hao walipowezakufanikiwa kumpora fedha hizo.
Wakati tukio hilo likitokea mmoja wa askari polisi wa Kituo cha Malindi Sajenti Hija Hassan Hija, alijaribu kupambana namabambazi hao, lakini alishindwa kufanikiwa baada na yeye kujeruhiwa sehemu ya mkononi na mguuni kutokana kushambuliwa kwa risasi.
Wakizungumza na gazeti hili, waathirika wa tukio hilo, Mfanya biashara Salum alisema, wakati alipokuwa akielekea maeneo ya Benki hiyo ndipo ilipotokea gari ndogo mbele yake na kumnadia mwizi na hapo ndipo walipompiga risasi ya mguu wa kulia na kumnyang’anya fedha hizo na kuondoka nazo .
Kwa upande wake askari Hija alisema, alipofika maeneo hayo ndipo alipomkuta Mfanyabiashara huyo akiwa katika harakati za kujinasua na hali na ndipo askari huyo alipokwenda kumuokoa lakini na yeye alishambuliwa na majambazi hao na kufanikiwa kuondoka na kitita hicho cha fedha zamfanyabiashara huyo,,
Hata hivyo, majeruhi hao bado wanaendelea kupata matibabu katika Hospitali kuu ya Mnazi mmoja na hali zao walieleza kuwa zinaendelea vizuri.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Mkadam Khamis Mkadam, alisema ni kweli tukio hilo limetokea na aliyeporwa fedha hizo ni Mfanyabiashara wa Mchele katika maeneo ya Bandarini ambae alikuwa akielekea katika Benki ya PBZ tawi la Mlandege.
Alisema mfanyabiashara huyo alikuwa na fedha zenye thamani ya shilling milioni 30,6,00,000, ambazo ni mali ya tajiri wake anafahamika kwa jina la Yussuf Mohamed, ambazo alikuwa anakwenda kuziweka katika Benki hiyo.
Hata hivyo, Kamanda Mkadam, alitoa wito kwa Wananchi wakati wanapokwenda kuweka pesa kuacha kwenda kwa miguu na kuwatumia askari kwani askari wapo kwa ajili yao ili kuimarisha usalama wa raia.
Sajenti Hija Hassan Hija, alijaribu kupambana na mabambazi hao, lakini alishindwa kufanikiwa baada na yeye kujeruhiwa sehemu ya mkononi na mguuni kutokana kushambuliwa kwa risasi.Akiwa katika hospitali ya Mnazi mmoja akjipata huduma ya kwanza.
Chanzo: zanzinews.com
Chanzo: zanzinews.com
ARSENAL CHUPUCHUPU KULIZWA NA TOTTENHAM LEO! #EPL
Nacer Chadli fired Tottenham into the lead in the north London derby
Alex Oxlade-Chamberlain akishangilia baada ya kuisawazishia timu yake goli katika dakika 74 ya mchezo.
Arsenal team: Szczesny, Chambers, Koscielny, Mertesacker, Gibbs, Arteta, Wilshere, Ozil, Chamberlain, Ramsey, Welbeck
Arsenal subs: Rosicky, Podolski, Ospina, Sanchez, Cazorla, Flamini, Coquelin
Spurs team: Lloris, Naughton, Kaboul, Vertonghen, Rose, Capoue, Mason, Lamela, Erikssen, Chadli, Adebayor
Spurs subs: Lennon, Soldado, Vorm, Dier, Townsend, Fazio, Bentaleb
Ratiba ya mechi kesho jumapili na jumatatu
Sunday 28 September 18:00West Brom v. Burnley
Monday 29 September 22:00Stoke v. Newcastle
RAMSEY, WILSHERE NA ARTETA WOTE NJE WIKI AU ZAIDI ARSENAL BAADA YA KUUMIA JANA DHIDI YA SPURS
KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger amethibitisha Aaron Ramsey, Jack Wilshere na Mikel Arteta wote watakuwa nje wiki ijayo- maana yake majeruhi hao wataukosa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Galatasaray Jumatani.
watatu hao wote wanatarajiwa kuukosa mchezo wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Chelsea Jumapili ijayo, baada ya kuumia jana katika sare ya 1-1 na Tottenham Hotspur Uwanja wa Emirates.
Wenger amesema: "Sifahamua muda mrefu kiasi watakuwa nje, lakini watakosekana wiki ijayo. Nafikiri Ramsey ni nyama (maumivu), na Arteta ni misuli ya nyuma ya mguu. Wilshere ni kifundo cha mguu,"amesema.
Friday, 26 September 2014
CRISTIANO RONALDO KUIGHARIMU MANCHESTER UNITED PAUNI MILIONI
GHARAMA halisi ya kumrejesha Cristiano Ronaldo Premier League inatajwa kuwa ni zaidi ya pauni milioni 140 huku pia ikigundulika kuwa washauri wa nyota huyo wa zamani wa Manchester United mkali huyo alipwe mshahara wa pauni milioni 20 kwa mwaka.
Inaelezwa kuwa Ronaldo hana amani Real Madrid na angependa kusikiliza ofa za kuondoka Bernabeu huku kocha wa Manchester United Louis van Gaal naye akishindwa kukanusha nia yake ya kumtaka mchezaji huyo bora wa dunia.
Hata hivyo klabu yoyote itakayomtaka Ronaldo italazimika kutoa mkwanja wa nguvu baada ya kubainika kuwa wawakilishi wa mchezaji huyo walitaka mshahara wa pauni 385,000 kwa wiki wakati alipotingisha kibiriti miezi 18 iliyopita.
Katika kipindi hicho, United chini ya David Moyes ilitaka saini ya Ronaldo ambapo familia ya Glazer ilikuwa imedhamiria kumrejesha nyota huyo lakini dili likashindikana.
Ronaldo akazivutia timu kadhaa barani Ulaya kabla ya kuamua kusaini mkataba mpya wa miaka mitano Bernabeu.
MWANAMAMA AFARIKI BAADA YA KUTOLEWA MIMBA KATIKA ZAHANATI MOJA YA MJINI IRINGA
MAMA mmoja (jina lake linahifadhiwa kwasasa) amefariki baada ya wahudumu wa zahanati moja ya mjini Iringa kujaribu kumtoa mimba bila mafanikio.
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea Jumatano ya wiki iliyopita katika zahanati hiyo iliyopo mjini hapa.
Baada ya taarifa hizo kuvuja, habari zilizoufikia mtandao huu zinaonesha kwamba Polisi walitia timu katika kituo hicho cha kutolea huduma jana na kuwakamata wahudumu wote waliokuwepo zamu katika Zahanati hiyo binafsi.
Wakati watoa huduma wakiachwa bila msaaada wowote katika selo ya Polisi Kati mjini Iringa,ndugu wa mkurugenzi huyo walifika na kumtoa mkurugenzi huyo baada ya kukamilisha taratibu za dhamana.
Mpashaji wetu amesema kabla ya kifo chake mama huyo alifika kituoni hapo akihisi ana ujauzito alioupata bila ridhaa yake.
Ili asitishe uhai wa kiumbe kilichoanza kuumbwa katika tumbo lake, mama huyo aliahidi kutoa sh 70,000 kwa mmoja wa watoa huduma wa zahanati hiyo ili atolewe mimba hiyo.
Kwa kuwa hakuwa na ujuzi, mtoa huduma huyo anadaiwa kutumia vifaa visivyotakiwa kutoa mimba hiyo hali iliyomsababishia mama huyo maumivu makali.
Hali ya mama huyo ilizidi kuwa mbaya baada ya kufika nyumbani kwake maeneo ya frelimo mjini Iringa.
Pamoja na ndugu wa mama huyo akiwemo mwanaume anayesadikika kuwa ni mumewe kumrudisha mama huyo katika zahanati hiyo, watoa huduma waliokuwepo zamu ya jioni ya siku hiyo aliyotolewa mimba, walihofia kumpokea kwa kile kinachoelezwa alikuwa katika hali mbaya.
Badala ya kumpeleka hospitali ya mkoa, ndugu hao walirudi na mama huyo nyumbani na taarifa zinaonesha kwamba alifariki saa moja baadaye.
Bada ya Polisi kunasa taarifa hizo walizuia mwili wa mama huyo usizikwe mpaka ulipofanyiwa uchunguzi na kubainika alikufa baada ya kukatwakatwa nyama za mlango wa uzazi wakati shughuli ya utoaji mimba ikiendelea.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi
anaendelea kutafutwa ili kuthibitisha taarufa hizi
BAWACHA YAPANGA KUMWONA KIKWETE KWA MAANDAMANO
Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha) limetangaza maandamano kwenda Ikulu kumuomba Rais Jakaya Kikwete asikubali kutia saini Rasimu ya Katiba inayopendekezwa iwapo itapitishwa na Bunge.
Mwenyekiti wa Bawacha, Halima Mdee alisema jana kwamba maandamano hayo yatafanyika mwishoni mwa wiki ijayo, baada ya maandalizi yatakayofanyika kwa siku saba kuanzia jana kukamilika.
Mdee ambaye pia ni mbunge wa Kawe, alisema baraza hilo limeamua kuitisha maandamano hayo ili kuwakilisha kilio cha wanawake ambao ndiyo waathirika wa kwanza pale nchi inapokuwa katika mfumo usio wa haki.
Alivitaka vyombo vya dola hasa polisi kujitokeza kuwasindikiza na kuandamana nao kwa kuwa nao ni miongoni mwa Watanzania ambao wataathiriwa na uamuzi usiolenga kujenga umoja wa kitaifa.
Hata hivyo, Polisi imetahadharisha kuwa itaendelea kuwachukulia hatua za kisheria wanachama wa Chadema watakaojiingiza katika maandamano yaliyopigwa marufuku nchini.
Msemaji wa Polisi, Advera Bulimba alisema, “Kauli yetu haijabadilika, maandamano ya Chadema ni batili. Yeyote atakayeandamana atakuwa anakiuka utii wa sheria bila shuruti. “Jukumu letu ni kuwalazimisha wote wasiotaka kufanya hivyo, kuitii kwa shuruti.”
Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaj Mussa Salum amewataka Watanzania kutokuwa na papara ya kupata Katiba Mpya kwani mwisho wa siku wenye uamuzi wa kutaka iwe ya namna gani ni wao.
“Ni vyema na busara Watanzania wakasubiri na kuliachia kazi Bunge hilo Maalumu ambalo linamaliza kazi hivi karibuni na wao kubaki na kazi ya kuchagua wanachokitaka kiwemo kwenye katiba hiyo.
Maandamano yazimwa
Polisi wamedhibiti wafuasi wa Chadema maeneo mbalimbali waliokuwa wamejipanga kufanya maandamano na wengine wamefikishwa kortini.
Wanachama zaidi ya 40 wa Chadema eneo la Mbalizi, Mbeya Vijijini walikumbana na virungu vya polisi muda mfupi baada ya kuanza maandamano katika Mtaa wa Z.
Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi alisema hakuwa na taarifa yoyote lakini angependa wakazi wa Mbeya wafikirie zaidi masuala ya elimu, biashara na kilimo kuliko siasa.
Katavi
Viongozi watatu na wafuasi 14 wa Chadema Mkoa wa Katavi wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kufanya maandamano bila kibali.
Wanachama hao walikamatwa jana saa nne asubuhi eneo la Zahanati ya Kasimba katika Mtaa wa Majengo A, wakiwa wanaandamana kwenda Viwanja vya Hoteli ya Mpanda walikopanga kufanya mkutano.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari alisema wanaoshikiliwa ni: Katibu wa Chadema wa Mkoa, Almasi Ntije, Mwenyekiti Wilaya ya Mpanda, Abraham Mapunda na Katibu wa Jimbo la Mpanda Mjini, Cretus Nkumba.
13 wanaswa Mwanza
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Valentino Mlowola amesema wanawashikilia watu sita baada ya kukutwa wamejikusanya katika makundi jambo lilioashiria walitaka kuandamana.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Mwanza, Adrian Tizeba alisema wanaoshikiliwa ni wanachama 13 na viongozi wao. Aliwataja baadhi ya viongozi wanaoshikiliwa kuwa ni Mwenyekiti wa Chadema Vijana Mkoa, Joseph Idd, Mwenyekiti Wilaya ya Nyamagana, Josephat Nungwana na Katibu wa Vijana Wilaya ya Ilemela ambaye hakumtaja.
Dar es Salaam
Wafuasi 12 Chadema wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka ya kufanya mkusanyiko usio halali kwa nia ya kuandamana.
Wakili wa Serikali, Bernard Kongola aliwataja washtakiwa hao mbele ya Hakimu Mkazi, Frank Moshi kuwa ni Paulo Stanley ‘Ndege’, Joseph Michael, Ajenta Emmanuel na Waziri Saidy ‘Mahunzi’.
Wengine ni Oldgard Lerio, Sifa Majura, Magreth Mapunda, Remina Peter, Stella Masanja, Mwanahamisi Hassani, Vaileth Seka na Sina Manzi.
Kongola alidai mahakamani kuwa juzi katika maeneo ya Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Ilala Boma walifanya mkusanyiko usio halali kwa nia ya kuandamana kinyume cha sheria.
Baada ya kusomewa mashtaka yanayowakabili, washtakiwa wote walikana na upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika.
Washtakiwa hao walirudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana na kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 8.
Subscribe to:
Posts (Atom)