Saturday, 6 September 2014

MANCHESTER UNITED KAMA WANA BAHATI VILE, ARTURO VIDAL AHARIBU TENA!


Kafungua ushindi: Arturo Vidal aliichezea Juventus ikishinda 1-0 dhidi ya Chievo katika mechi ya Seria kabla ya mapumziko ya kupisha mechi za kirafiki za kimataifa.
MANCHESTER United wameonekana kuwa na bahati ya kujiepusha na majanga baada ya mchezaji waliyemuwania kwa muda mrefu majira ya kiangazi mwaka huu, Arturo Vidal kupata majeruhi tena ya goti akiwa katika mazoezi ya timu ya Taifa ya Chile kujiandaa na michezo miwili ya kimataifa ya kirafiki iliyopo katika kalenda ya FIFA.
Nyota huyo wa Juventus aliondoka mazoezini mjini Miami ambapo Chile itakabiliana na Mexico na Haiti katika mechi za kirafiki, lakini anategemewa kufanyiwa vipimo vikubwa kabla ya kurudi Italia.
Vidal kwa muda mrefu alikuwa akihusishwa kujiunga Old Trafford majira ya kiangazi, lakini dili hilo halikuweza kukamilika licha ya mazungumzo ya mara kwa mara baina ya klabu hizo mbili kufanyika.
Nyota huyo mwenye miaka 27 alifanyiwa upasuaji wa goti mwishoni mwa msimu uliopita na alionekana kuwa fiti katika michuano ya kombe la dunia.
Kocha wa Manchester United, Louis van Gaal alivutiwa na kiungo huyo, lakini ada yake ilikuwa kubwa sana, ingawa ukweli ni kwamba alihofia hali ya mchezaji huyo kwasababu hakuwa fiti kabisa.
Taarifa zinasema Vidal anaweza kufanyiwa upasuaji mwingine tena.

No comments:

Post a Comment